Zaburi 42:1

Kama paa atamanivyo maji ya kijito,ndivyo ninavyokutamani ee Mungu wangu...!!.

Zaburi 42:2

Naona kiu ya Mungu,kiu ya Mungu alie hai,nitafika lini kwake na kuuona uso wake..?.

Zaburi 42:3

Machozi yamekuwa chakula changu mchana na usiku,waliponiambiakila siku 'yuko wapi Mungu wako?'.

43:4

Nakumbuka tena mambo haya kwa majonzi moyoni mwangu:Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu,nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Mungu wakipiga vigelegele vya shukrani;umati wa watu wakifanya sherehe!.

Zaburi 42:5

Mbona nasononeka hivyo moyoni? Kwa nini nahangaika hivyo ndani mwangu? Nitamtumainia Mungu, maana nitamsifu tena yeye aliye msaada wangu na Mungu wangu

Thursday, 29 June 2017

DALILI ZA MTU ALIYE NA JINI MAHABA NA UVAMIZI WA MAJINI MBALIMBALI WENYE UHARIBIFU. NA NAMNA YA KUOMBA AU KUOMBEA ILI KUFUNGULIWA KWENYE VIFUNGO VYA MAJINI. MLIMA MTAKATIFU MINISTRY TANZANIA ( MMMT)


Bwana Yesu apewe sifa wapendwa!!!. UFUNUO WA YOHANA 12:7:12. Kulikua na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbingu 12 ……… Ole wa nchi na bahari kwa maana yule lbilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi akijua yakuwa ana wakati mchache, Vita hii ndio lnayoendelea juu ya malaika wa shetani ambao ndio majini, mapepo, kupitia waganga wa kienyeji na wachawi, hapa hakuna cha jini mzuri wa baya majini wote ni wabaya kwa maana walimuasi muumba wao pamoja na lusifa ambaye alikuwa malaika wa sifa huko mbinguni naye akataka kupindua selikali ya ufalme wa Mungu muumba mbingu na nchi, baada ya kushindwa akatupwa huku chini makao ya lusifa ni kuzimu na malango yake yapo baharini, kila nchi lna malango ya kuzimu.
HIZI NDIO DALILI ZA UWEPO WA JINI MAHABA NDANI YA MWANADAMU AU MAJINI AINA NYINGINE WAHARIBIFU KAMA WANAVYOTUMWA NA MAWAKALA WENGINE WACHAWI NA WAGANGA.
1)  kuwashwa washwa mwilini kama vitu vinakutembea tembea
2) kuwaka tama sana ya ngono pindi unapokua peke yako lakin unapokua na mweza wako hamu hutoweka. Mwanaume hupoteza nguvu.
3) kuhisi au kuota unalala na mtu kitandani
4) Mwili kusisimuka mara kwa mara hasa sehemu kuanzia kiunoni kushuka chini.
5) Kutamani kua na mweza wako pindi anapokua mbali lakin akiwa karibu humchukia bila sababu za msingi.
6) Kua na hasra sana bila hata sababu za msingi
7) Kuwa na hali ya kutojali au kuthaminni wengine umimi na kujiona wa thamani peke yako kuliko wengine.
8) Kuchukiwa na ndugu jamaa na marafiki anakufanya ufanye mambo yakuchukiza wengine
9) Kujiona mtu mwenye mikosi nuksi na balaa tupu
10) Kuvurugika kwa mipango/ mambo yako/ hasa ya maendeleo na kila unachopanga hushindikana hata kama ukisaidiwa na mwisho hujiona hufai
11) Kuumwa kichwa pindi wakat unasoma Biblia au masomo ya kawaida
12) Kutokujisikia kuomba au kusinzia pindi unapotaka kuanza maombi, huishiwa nguvu kabisa, Na kuishia kuhangaika kama mtu asiyejua lakufanya
13) Kuota lbada zisizoeleweka
14) Kuota ndoto za kutisha kama unafukuzwa na watu, Mnyama , Nyoka au kuota unaanguka kwenye shimo lefu lakin hufiki chini, Mafuriko ya maji mengi na wakat mwingine maji haya huwa machafu na ndani yake kua na nyoka
15) Kuota upo kando kando ya bahari, katka mto, au porini, Sherehe za harusi, harusi au ya mtu usiyemjua lla mnakula
16) kuota una mimba au unajifungua, una mtoto
17) Kujisikia umechoka masaa yote, na kutamani kulala masaa yote kutokujisikia kufanya chochote. Kuhisi uzito wa mwili kama umebeba kitu kizito
17)  Maumivu chini ya kitovu kwa akina mama au katka mji wa uzazi
18) Kusikia maumivu makari wakat wa tendo la ndoa kwa akina mama
19) Kujihisi unaingiliwa na mwanaume au unalala na mwanamke mara kwa mara
20) Mimba kuharibika bila sababu za msingi, Kufunga hedhi bila sababu. Hizi tu ni badhi ya dalili za kuwepo jini mahaba ndani ya mwanadamu, sio lazma uwe nazo zote hapana, lakin pia sio hizi peke yake zipo nyingi sana. Na ndio maana.             LINDA SANA MOYO WAKO                  Biblia lnatuhimiza kuulinda moyo kuliko kito chochote kile Mithali 23:26. Ukishindwa kuulinda moyo wako nirahisi sana kutawaliwa na jini Mahaba au kashikashi, na madhara yakutawaliwa na viumbe hawa ni makubwa sana.  kichwa NAMNA YA KUMFUNGUA MWENYE PEPO MAHABA AU KASHIKASHI AU AINA YOYOTE YA MAJINI. = Viumbe hawa ni viumbe wasionekana, maana yake ni roho hawaonekani kwa umbo la kibinamu japo wana uwezo wakujigeuza chochote. na mara nyingi hutumwa na wachawi, na waganga ili kumdhuru mtu au kumharibia au kumtumikisha, kwasababu ya wivu au kutafuta utajiri, lakini pia wanapokupenda wenyewe huingia ndani yako na kufanya makao, ndani yako haswa kwa wale ambao hawajaokoka, yaani kumpa Yesu maisha yako au hata kama umeokoka lakin njia zàko si njema mbele za Mungu. NJIA YA KUEPUKA MATESO YA VIUMBE HAWA NI UTAKATIFU NA IBADA, MAOMBI YA MARA KWA MARA. viumbe hawa ni mawakala  shetani, Ibilisi, joka lusifa hawa ndio malaika walioasi pamoja na lusifa baada ya kupigwa mbinguni na kutupwa huku sasa wanapambana na wanadamu. ( tafakari kwa kina mistr hii) UFUNUO WA YOHANA 12:7-12. Mstr wa 7 Unasema kulikua na vita mbinguni Mikaeli na Malaika wakapigana na yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake 8 Nao hawakushinda wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Mstr 12 ………… Ole wa nchi na bahari kwa maana yule lbilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi akijua kuwa ana wakati mchache. = Hawa malaika wanaotajwa hapa kama malaika wa shetani ndio majini na mapepo nk. NAMNA YA KUOMBA ILI KUFUKUZA VIUMBE HAWA NDANI YA MWANADAMU (1)Omba toba kwa Mungu ili akusamehe dhambi zote ambazo umezifanya kwa mwili pamoja na rohoni yaani dhambi kupitia ndoto chafu, Omba toba kwa ajili ya madhara ambayo umeyata kwenye ulimwengu wa roho lkiwa kuzaa au kuzalisha watoto wa majini,kupandikizwa umasikini, roho za uzinzi na umalaya, nk Omba toba kwa ajili ya familia na ukoo kama kuna mwingilianon wowote, au kurithishwa kutoka kwenye familia na ukoo lsaya 43:25 Zaburi 51. toba ni njia ya kutafuta utakatifu mbele za Mungu aliye hai. KARIBISHA UWEPO WA MUNGU baada ya toba  Mathayo 6:9-10=Unashusha ufalme wake Mungu. Unamwita Mungu kwa maana yeye anasema niite nami nitaitika Yeremia 33:1-3/6 OMBA MWONGOZO WA ROHO MTAKATIFU. Jifunike kwa damu ya Yesu funika ndugu jamaa na marafiki kazi biashara kila kitu ambacho unajua kinaweza kushambukiwa na shetani wakati unaomba au kumwombea Mtu funika kwa damu ya Yesu. Vaa silaha za Mungu Waefeso 6:11-18 maana vita hii sio ya damu na nyama bali ni katika ulimwengu wa roho juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza yaani (Wachawi na waganga,) na majeshi yaani (majini yenyewe) na mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho kuanzia mstr wa 13 ndio silaha zenyewe. Hakikisha una uhakika na kile unachofanya maana lmani ni hakika ya mambo ya tarajiwayo ni bayana ya mambo ya siyoonekana. Maana lngawa tunaenenda kwa mwili hatufanyi vita jinsi ya mwili, ( maana silaha za vita vyetu si vya mwili, bali zinauwezo katika Mungu hata kuangusha ngome 2 Wakorintho 10:1-6  Kwa jina la Yesu!!! anza Kuvunja mikataba na na maagano uliyoingia kwa njia ndoto, kama uliota unafunga ndoa vunja, kama uliota mjamzito na kisha kujifungua mpaka unanyonyesha vunja, peleka moto wa Yesu mwaga damu ya Yesu. Vunja mikataba yote uliyofungamanishwa nayo, na mikata hii wanaweza kukufungisha ndoa na jini chini ya bahari au njia panda au kwenye miti milefu au kwenye milima au angani, Mungu aliyeumba mbingu na nchi ni moto ulao lta moto kwa jina la Yesu Kristo vunja hiyo mikaba yote ya ndoa, Umaskin kutumikishwa nyota yako kutumika kichawi, vifungo vyote vifunguwe kwa damu Yesu kamba zote za kichawi katakata kwa upanga wa neno la Mungu maana neno la Mungu ni upanga ukatao kuwiri, Vunja kila madhabahu  lnayokushikilia, lwe ya mizimu, yakichawi, yamapepo vunja Yeremia 1:9-10. Mungu amekufanya wewe kuwa kuhani na mfalme naye amekuweka juu ya falme zote ili kung' oa na kubomoa, na kuharibu na kuangamiza, ili kujenga na kupanda tena, kwa ondoa ufalme wa shetani ndani yako, familia yako ukoo wako kisha jenga ufalme wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Umepewa mamlaka ya kukanyaga joka na nge na nguvu zote za muovu shetan Luka 10:19 Achiliya moto juu ya jini Tajirini kama walitaka kukuchukua kafara,ili wapate utajiri tuma moto wa Yesu. achilia moto juu ya jini Muzafari maana huyu ndio huzuia mafanikio achiliya moto juu ya jini Anzura na Shamsu hawa ndio hufukuza wachumba nakukufunga usiowe au kuolewa, achilia moto juu ya jini Amri huyu ndio huleta ugomvi na kusababisha hasra ili kufungua mlango wa mapepo kuingia ndani yako, Funga milango yote kwa damu ya Mwana- kondoo Ufunuo 12:11, piga kwa moto ulao kama jini Tsemlee kama mimba zilikua zinaharibika hovyo,; piga moto jini Subiani kama ulikuwa huoni siku zako au zilikua zinatoka mfululizo au kidogokidogo maana huyu ndi mnywaji wa damu na husababisha ajari, piga jini Jahadi huyu ni chuma ulete anaiba pesa piga jini Latifa huyu analeta ufukura kwenye maisha, piga jini Sifariru huyu ni jini kahaba anawashawishi watu kufanya uzinzi na umalaya piga jini Maimuna kama ulikua unasikia maumivu chini ya kitovu na kuota unafanya mapenzi, WAKATI UNAFANYA HAYA YOTE USISAHAU DAMU YA MWANAKONDO MAANA MIKAELI ALISHIMNDA SHETANI KWA DAMU YA MWANA KONDOO Piga jini Ratafari kama unafuatiriwa na laana za ukoo, piga jini Janjatusi hili ndio linawafanya watu kulala usingizi wakati wa mahubiri, teketeza kwa moto ulao kila kiumbe kutoka kuzimu katika jina la Yesu vunja madhabahu zote kwa damu ya Yesu achilia damu ya Yesu lkafanyike fidia juu ya kila sadaka waliopewa majini na waganga haribu kazi zote za kishetani peleka moto kwenye malango ya kuzimu wachiye jina lako na nafsi yako, kwa jina la Yesu vunja vikao vyote vinavyokaliwa kwa ajili yako na familia. Mshukulu Mungu ukitaja majina yake kama ahsante Mungu mkombozi Mungu wa lbrahimu lsaka na yakobo, Mungu mwenye enzi, Mungu usiyeshindwa Ebeneza Jehova shalom au lmba nyimbo za sifa huku ukiamini kwamba umefunguliwa, maana neno linasema lolote mwombalo amini kuwa mmepokea nayo yatakuwa yenu, kabula ya kufanya maombi haya unaweza kufanga saa 24 au siku tatu masaa 12 kila siku ltategemea na msukumo wako, lakin kufunga sio njia ya kumshawishi Mungu kujibu maombi bali ni njia yakutafuta nguvu za rohoni maana vita ya majini mapepo, na wachawi ni ya rohoni zaidi MUNGU AKUBARIKI SANA. NI MIM NDUGU YAKO KATKA KRISTO YESU MT S M MENDULO. KWA mawasiliano kwa ajili ya maombi na maombezi na. Mafundisho ya lnjili ya Yesu kuhusu ufalme wa mbinguni na msamaha kamili wa dhambi zote nipigie +255656995917 au email samendulo@gmail.com or Mlimamtakatifumistry@gmail.com. Tupo Kinondoni, Goba, Mabibo, NYOTE MNAKARIBISHWA Amen.

Wednesday, 9 March 2016

MUNGU WA KWELI HUJITAMBULISHA MWENYEWE

SHALOM!!!!
BWANA YESU APEWE SIFA!!!Mpendwa katka Kristo Yesu aliye Mwana wa Mungu ambaye ndio kifo chake kimetupa haki ya kwenda mbele za Mungu moja kwa moja kupitia jina lake ambalo ni zaid ya majina maana kwa Jina la Yesu lazma kila goti lipigwe!!!
Mpendwa wangu nina matumaini yakua umzima na kama ni mgonjwa pokea uponyaji kwa jina la Yesu.
Karibu tujifunze somo hili ambalo lina kichwa
MUNGU WA KWELI HUJITAMBULISHA MWENYEWE
Sehemu yoyote au mahali popote ambapo Mungu yupo na Mungu huyo ndio muumba vyote huwezi kutumia nguvu wala mapanga au silaha, maana Mungu hujitambulisha mwenyewe kwa matendo yake makuu tena na utisho mkubwa. Kiasi chakwamba hata yule ambaye alikua anaabudu Mungu mwingine tofaut na Mungu aliyeumba mbingu na Nchi lazma akili yakwamba huyu ndio Mungu wa kweli.
YONA 1:1-17
Biblia lnatufundisha habari za Mtumishi wa Mungu Yona lnaeleza kuhusu maagizo ambayo Yona alipewa kutoka kwa Mungu lakin Yona alikaidi maagizo hayo ukisoma mstr wa kwanza na wa pili Unasema Basi neno la Bwana lilimjia Yona mwana wa Amitai kusema,(2) Ondoka uende Ninawi mji ule mkubwa ukapige kelele juu yake kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
Lengo la Mungu alitaka Yona aende ule mji akahubiri habari njema za Mungu ili watu wa ninawi watubu nakuacha njia zao mbaya wapate kumrudia Mungu lakin Yona alitowa hukumu ndani ya moyo wake kwa maana hakutaka waninawi wasamehewe kwa maana maovu yao yalikua makubwa.
Ndipo Yona akaondoka kuelekea Tashrshi ili kujiepusha na Bwana lakin Mungu hakutaka kumwacha Yona naye aende alimfuata mpaka alikokua anaelekea mstr wa, (4) Unasema Lakin Bwana alituma upepo mkuu Baharin lkawa tufani kubwa baharini, hata merikebu lkawa karibu kuvunjika mstr 5) ambao ndio point yetu ya msingi unasema, basi wale mabaharia wakaogopa kila mtu akamwomba mungu wake nao wakatupa baharini shehena iliyojua merikebuni ili kupunguza uzito wake lakin Yona alikua ameshuka pande za ndani ya merikebu akajilaza akapata usingizi .


Kwenye mistr hii miwiri hasa mstr wa (5) Unasema Basi mabaharia wakaogopa kila mmoja akamwomba mungu wake,- Katka mstr huu tunaona kwamba kila baharia alikua na Mungu wake na kila mmoja alimwomba huyo Mungu lakin tufani haikutulia Kwa maana Mungu wa Yona ambaye ndiio Mungu mkuu ndio aliyechafua bahari. Na Yona kwakujua hayo kwamba tufani ni kwa ajili yake alienda pande za chini na kuuchapa usingizi bila waswas wowote. Mpendwa huenda na wewe ndio cha matatizo katka familia yako kwa maana umekimbia kazi ya Mungu nakushauri rudi umpokeye Yesu. Lakin katika yote Yona alipouliza alikubali kwamba tufani ni kwa ajiri yake naye akachaguwa wamtupe baharin. Mstr wa 13 unaonyesha mabaharia wakimlilia Bwana na hapa ni baada ya kugundua kua yupo Mungu mkuu zaid ya miungu waliokua wakiabudu na kuiomba kabla ya tufani, mstr wa 15 unasema basi wakamkamata Yona nakumtupa baharini nayo bahari lkaacha kuchafuka mstr wa 16 ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno wakamtolea Bwana sadaka na nadhiri
Watu hawa ambao ni mabaria waligundua uwepo wa Mungu ambaye nimuweza wa yote baada ya kuona matendo makuu na pale pale walikiri nakuanza kumwomba na baada ya kumtupa Yona baharin na bahari kunyamaza ndipo wakaogopa tena wakamtolea Bwana sadaka na kuweka nadhiri. Mpendwa ninakuambia katka jina la Yesu yakwamba MUNGU HUJITAMBULISHA MWENYEWE.
>>> Nakukaribisha katka huduma ya Maombi Nyumbani kwa Mzee Magongo Kinondoni Mkwajuni. Tunatazamana na nyumba ya Diwani Mhe Kimbita. Njoo tumuombe Mungu kwa pamoja naye atakufungua naye atajidhihirisha kwako kama alivyojidhirihidha kwa mabaharia, kupitia neno lake pamoja na maombi. Kwa mawasiliano zaidi tuma msg au piga +255656995917 Goba unashuka kituo cha Contena halaf piga cmu.
>> Mungu akubariki sana Amen<<




Friday, 4 March 2016

KUSONGA MBELE LAZIMA.








SHALOM!!!
Ninamshukulu Mungu aliyeumba mbingu na nchi kwakua ameifanya siku ya leo, Naye ameniamsha vyema kabsa, Sifa na utukufu ni kwako Bwana Mungu wa majeshi uliye muweza wa yote Amen.
Mpendwa katka Kristo Yesu karibu Tujifunze jambo kwakua sote tumefanyika wanafunzi wa Yesu.


Yamkini upo katka hali ambayo bado hujapata majibu yakwamba mwisho wake nin juu ya jambo ambalo linakutatiza. Katka maisha kuna mapito mengi, majaribu nayo nimengi, lakin kwa jina la Yesu ninakwambia
KUSONGA MBELE LAZIMA
huenda usielewe kwanini ninasema kusonga mbele lazma, lakin nikwakua wewe sio wa kwanza kupitia magumu, mapito na majaribu unayopitia, walikuwepo watu walipitia magumu na mateso mengi lakin kwa msaada wa Bwana waliweza kushinda. Hata kama ni vita ya kiroho lazma ujuwe kwamba ni mpila peke na michezo mingine ndio wanaweza kupata droo kwa maana ya kutofungana, au kufungana magoli yaliyo sawa, lakin vita ya kiroho lazma awepo mshindi na siku zote Elishadai Jehova ndio Mungu asiye shindwa. Haleluyaaaaaa!!!!!
Biblia katka kitabu cha Kutoka 14:11-16 lnatueleza habar za wana wa lsrael na jeshi la Farao, wana wa lsrael waliona bahari ya shamu mbele yao, Nao walikata tama walijua mwisho wao umefika, Ndipo wakanung'unika mbele ya Musa. Wakasema mstr wa 11 Kwasababu hapakua na makaburi katka Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mpendwa nawe huenda unajiuliza maswali mengi juu ya hatma yako, huenda umefika wakat unasema Mungu amekuacha lakin lipo neno la matumaini kwako bado kwa maana Mungu hajakuacha. Mstr wa 13  Musa anawambia
Msiogope simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele (14)  Bwana atawapigania ninyi nanyi mtanyamaza kimya. Jina la Bwana libarikiwe sana
Mpendwa katka Kristo Yesu Musa wakat anasema maneno haya yeye mwenyewe hakujua Mungu atawaokowa vip na ataanzia wap? Lakin yeye alimwamini Mungu kwamaana alijua safari yao lmepangwa na Mungu. Nami nakueleza yakwamba huenda hujui na huelewi yakwamba Mungu atakupigania vip na ataanzia wap lakin yeye ni Bwana wa majeshi naye ni mshindi!!! Sema Amina! Kubwa!!! Licha ya Musa kusema kwa ujasiri lakin hakujua ni wapi nayeye anziye na ndio maana mstr wa (15) Mungu anamwambia Musa Bwana akamwambia Musa mbona wanililia mim? Wambie wana wa lsraeli waendelee mbele. Hoo haleluya Mungu anamwambia Musa kwa nin unanililia? Kumbe Musa naye wakat anasema maneno yale alikua akilia ndani ya moyo wake lakin kilikua nikilio cha kumwomba Bwana na sio kilio cha kunung'unika kama wana wa lsraeli walivyolia Musa alikuwa akisema tusaidie Bwana usituache!! Lakin alisahau yakwamba anayo fimbo mkononi mwake. Lakin cha ajabu Mungu anamwambia Musa wambie wana wa lsraeli WAENDELEE MBELE, YANI WASONGE MBELE. sio kwamba Mungu hakuiona bahari aliona lakin anasema WAENDELEE MBELE. KUSONGA MBELE nami kwa jina la Yesu Kristo wa nazaret aliyekufa kwa ajili yako na yakwangu nakwambia lazma usonge mbele hata kama mbele kuna bahari hata kama huna matumaini, hata unaona ukuta lakin Kusonga mbele lazma. Kwa maana yupo Bwana wa Majeshi naye anayaona unayopitia naye atatenda mambo makubwa juu yako nawe utanyamaza kimya. Musa anaambiwa lnua fimbo yako, ukanyoshe mkono waki juu ya bahari na kuigawanya nao wana wa lsraeli watapita kati ya bahari katka nchi kavu. Mungu alitenda muujiza mkubwa ambao wana wa lsraeli hawakutegemea nami nakushauri endelea kuomba endelea kuomba wala usichoke maana upo muujiza mkubwa mbele yako. Biblia lnasema katka kitabu cha
Isaya 40:28-31Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, muumba miisho ya dunia, hazimii wala hachoki akili zake hazichunguziki 29 Huwapa nguvu wazimiao humwongeza nguvu yeye asiye na uwezo. Akili za Mungu hazichunguziki Dada yangu, kaka yangu, Mama yangu mdogo wangu kwa maana wakat wewe unaona bahari kama wana wa lsraeli yeye anaona nchi kavu ndani ya bahari.KUSONGA MBELE LAZMA  NDUGU kwa maana lipo neno la matumaini kutoka katka kitabu cha
Isaya 43:1-3  Umeitwa kwa jina lako upitapo katka maji mengi nitakuwa pamoja nawe, na katka mito haitakugharikisha uendapo katka moto hauteketea wala mwali wa moto hautakuunguza. Hoo!!Haleluya!!!!! Maana yeye ni Bwana Mungu wako ninakwambia kusonga mbele lazma na ni marufuku kukata tama. Kwa maana Bwana anakupa uhakika wakukutetea. Ubarikiwe sana.
By Samuel M Mendulo
Samendulo@gmail.com.
Namba +255656995917 Amen

Juma la 3 la kwaresma


Alhamisi 3 2016
Somo la 1
Yer. 7:23-28

Naliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru, mpate kufanikiwa. Lakini hawakusikiliza, wala kutega sikio lao, bali walikwenda kw amashauri yao wenyewe, na kwa ushupavu wa mioyo yao mibaya, wakaenda nyuma wala si mbele. Tokea siku ile baba zenu walipotoka katika nchi ya Misri hata leo, nimewatuma watumishi wangu wote manabii kwenu ninyi, nikiamka mapema kila siku na kuwatuma. Lakini hawakunisikiliza, wala kutega sikio lao; bali walifanya shingo yao kuwa ngumu; walitenda mabaya kuliko baba zao. Nawe utawaambia maneno hayo yote; lakini hawatakusikiliza; nawe utawaita; lakini hawatakuitikia. Nawe utawaambia, Taifa hili ndilo lisilosikiliza sauti ya Bwana, Mungu wao, wala kupokea mafundisho; uaminifu umepotea, umekatiliwa mbali vinywa vyao,

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 95:1-2, 6-9 (K) 7

(K) Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu.

Njoni, tumwimbie Bwana,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi. (K)

Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake. (K)

Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Msifanye migumu mioyo yenu;
Kama vile huko Meriba,
Kama siku ya Masa jangwani.
Hapo waliponijaribu baba zenu,
Wakanipima, wakayaona matendo yangu. (K)

SHANGILIO
Zab. 51:10, 12

Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Unirudishie furaha ya wokovu wako.

INJILI
Lk. 11:14-23

Yesu alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo alipotoka, yule bubu akanena, makutano wakastaajabu. Wengine wao wakasema, Atoa pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo. Wengine walimjaribu, wakitaka ishara itokayo mbinguni. Naye akajua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka. Basi, ikiwa Shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli, wana wenu je! Huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo, hao ndio watakaowahukumu. Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang?anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.
Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.

Wednesday, 2 March 2016

BADHI YA DALILI ZA KUA NA JINI MAHABA AU KASHKASH NDAN YA MWILI WA MWANADAMU

Bwana Yesu apewe sifa wapendwa!!!

1)  kuwashwa washwa mwilini kama vitu vinakutembea tembea
2) kuwaka tama sana ya ngono pindi unapokua peke yako lakin unapokua na mweza wako hamu hutoweka. Mwanaume hupoteza nguvu.
3) kuhisi au kuota unalala na mtu kitandani
4) Mwili kusisimuka mara kwa mara hasa sehemu kuanzia kiunoni kushuka chini.
5) Kutamani kua na mweza wako pindi anapokua mbali lakin akiwa karibu humchukia bila sababu za msingi.
6) Kua na hasra sana bila hata sababu za msingi
7) Kuwa na hali ya kutojali au kuthaminni wengine umimi na kujiona wa thamani peke yako kuliko wengine.
8) Kuchukiwa na ndugu jamaa na marafiki anakufanya ufanye mambo yakuchukiza wengine
9) Kujiona mtu mwenye mikosi nuksi na balaa tupu
10) Kuvurugika kwa mipango/ mambo yako/ hasa ya maendeleo na kila unachopanga hushindikana hata kama ukisaidiwa na mwisho hujiona hufai
11) Kuumwa kichwa pindi wakat unasoma Biblia au masomo ya kawaida
12) Kutokujisikia kuomba au kusinzia pindi unapotaka kuanza maombi, huishiwa nguvu kabisa, Na kuishia kuhangaika kama mtu asiyejua lakufanya
13) Kuota lbada zisizoeleweka
14) Kuota ndoto za kutisha kama unafukuzwa na watu, Mnyama , Nyoka au kuota unaanguka kwenye shimo lefu lakin hufiki chini, Mafuriko ya maji mengi na wakat mwingine maji haya huwa machafu na ndani yake kua na nyoka
15) Kuota upo kando kando ya bahari, katka mto, au porini, Sherehe za harusi, harusi au ya mtu usiyemjua lla mnakula
16) kuota una mimba au unajifungua, una mtoto
17) Kujisikia umechoka masaa yote, na kutamani kulala masaa yote kutokujisikia kufanya chochote. Kuhisi uzito wa mwili kama umebeba kitu kizito
17)  Maumivu chini ya kitovu kwa akina mama au katka mji wa uzazi
18) Kusikia maumivu makari wakat wa tendo la ndoa kwa akina mama
19) Kujihisi unaingiliwa na mwanaume au unalala na mwanamke mara kwa mara
20) Mimba kuharibika bila sababu za msingi, Kufunga hedhi bila sababu. Hizi tu ni badhi ya dalili za kuwepo jini mahaba ndani ya mwanadamu, sio lazma uwe nazo zote hapana, lakin pia sio hizi peke yake zipo nyingi sana. Na ndio maana Biblia lnatuhimiza kuulinda moyo kuliko kito chochote kile Mithali 23:26. Ukishindwa kuulinda moyo wako nirahisi sana kutawaliwa na jini Mahaba au kashikashi, na madhara yakutawaliwa na viumbe hawa ni makubwa sana. Itaendelea  kichwa NAMNA YA KUMFUNGUA MWENYE PEPO MAHABA AU KASHIKASHI.
Samuel M Mendulo
Samendulo@gmail.com
Namba +255656995917

Friday, 26 February 2016

YESU ANAKUITA



Mwito wa Yesu ,(wito nikitendo cha kumsikia Mungu akitoa majukumu ya Utumishi wako)

Hadi unaitwa ujue ulikuwa kwenye mpango wa Mungu tangu hujazaliwa.

YEREMIA 1:5  Mungu ana sema , ?KABLA SIJA KUUMBA KATIKA TUMBO NALIKUJUA, NA KABLA HUJATOKA TUMBONI, NALIKUTAKASA; NIMEKUWEKA KUWA NABII WA MATAIFA. ?

Sasa basi hilineno lililomjja Yeremia lilikuwa ndiyo Yesu ( Neno=Yesu)

YOHANE 1:1-12 Point ipo 1:1?HAPO MWANZO PALIKUWEPO NENO,  NAYE NENO ALIKUWAKO KWA MUNGU, NAE NENO ALIKUWA MUNGU. ?

Hata leo Yesu anatuita tutende kazi yake yaani tutende mapenzi ya Baba.

YOHANA 6:38 Yesu anasema ?KWAKUWA MIMI SIKUSHUKA TOKA MBINGUNI ILI NIFANYE MAPENZI YANGU, BALI MAPENZI YAKE ALIE NIPELEKA.

Kama yeye amekuja kutimiza mapenzi ya Baba,  basi ni dhahiri kuwa anataka na wewe uyatimize vivyo hivyo,  yaani utumike kutimiza mapenzi ya Baba ila kupitia yeye.?

Mwitohuu hauchagui hali wala mali, bali yeyote atakaetii sauti hiyo, ZABURI 95:8 ?
MSIFANYE MIGUMU MIOYO YENU KAMA HUKO MERIBA KAMA SIKU YA MUSA JANGWANI,? mkisikia sauti ya Roho mtakatifu WAEBRANIA 3:7-8 ?KWAHIYO KAMA ANENAVYO ROHO MTAKATIFU, LEO KAMA MTAISIKIA SAUTI YAKE, MSIFANYE MIGUMU MIOYO YENU, KAMA WAKATI WA KUKASIRISHA , SIKU YA KUJARIBIWA KATIKA JANGWA,?

kumbuka Dhumuni kubwa ni wewe kutumika ili kazi ya Mungu ifanyike kupitia wewe YEREMIA 51:20-23, nitakuonesha mstar wa 20,?WEW U TLRUNGU LANGU NA SILAHA ZANGU ZA VITA,  KWA WEWE NITAVUNJA VUNJA MATAIFA ,  NA KWA WEWE NITAHARIBU FALME. ?

Katika wito huu pia Mungu anatuhakikishia usalama katika kutenda kazi nae ! YOSHUA 1:9 ?
JE!  SI MIMI NILIE KUAMURU?  UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA;USIOGOPE WALA USIFADHAIKE;KWAKUWA BWANA MUNGU WAKO,  YU PAMOJA NAWE KILA UENDAKO. ?

Nakila silaha ya kufanya kazi tunayo, 2PETRO 1:3 ?KWAKUWA UWEZA WAKE WA UUNGU UMETUKIRIMIA VITIVYOTE VIPASAVYO UZIMA NA UTAUWA, KWAKUMJUA YEYE ALIETUITA KWA UTUKUFUWAKE NA WEMA WAKE MWENYEWE?, Kwahiyo tunakila sababu ya kutii,  Yeremia alisema YEREMIA 1:6  ?NDIPO NILIPOSEMA, AA,  BWANA MUNGU! TAZAMA SIWEZIKUSEMA MAANA MIMI NI MTOTO?. na Mungu akamjibu YEREMIA 1:7-87-8 ?LAKINI BWANA AKANIAMBIA USISEME, MIMI NIMTOTO;MAANA UTAKWENDA KWA KILAMTU NITAKAE KUTUMA KWAKE, NAWE UTASEMA KILA NENO NITAKALO KUAMURU, USIOGOPE KWA SABABU YA HAO MAANA MIMI NIPO PAMOJA NAWE NIKUOKOE, ASEMA BWANA.?

Tujifunze kukubali wito na tusali sala ya kushukuru na kupokea ule wito tulio itiwa. Marium alipewa wito wa kuchukua mimba na kumzaa Yesu ambae leo nimkombozi wetu,  katika mwito ule yeye  ali uitikia na kuupokea kikamilifu,  LUKA 1:38 ?MARIUM AKASEMA ,  TAZAMA MIMI NI MJAKAZI WA BWANA NAIWEKWANGU KAMA ULIVYOSEMA . KISHA MALAIKA AKAONDOKA AKAENDA ZAKE.?  lakini tukirudi nyuma kidogo LUKA 1:26-37.  Utaona Marium aliuliza masali ili kufahamu wito wake kisawasawa,  hata wewe waweza kusali na kumuuliza Mungu ili akufunulie na kukufanya uujue,   Waefeso 1:17-23 point ipo kwenye 18, ?
MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU, MJUE TUMAINI LA MWITO WAKE JINSI LILIVYO, NAUTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHIWAKE KATIKA WATAKATIFU  JINSI ULIVYO?

Sasa basi Yesu anatuita kwenye wito ili tujenge kanisa ambalo yeye mwenye ndio kichwa cha kanisa lenyewe, WAKOLOSAI 1:18 ?
NAE NDIO KICHWA CHA MWILI YAANI CHA KANISA,NAYE NI MWANZO , NI MZALIWA WA KWANZA KATIKA WAFU, ILIKWAMBA AWE MTANGULIZI KATIKA YOTE. ?

Yesu alipotoka jangwani kujaribiwa alianza kwa kuwaita wale mitume Mathayo 4:18-21 ,  ambao waliongozana nae katika kutenda kazi, kazi yao kubwa ilikuwa kufanya kazi na Yesu pamoja na kujifunza kumjua Mungu kupitia Yesu,

Nahawa aliowateuwa kuwa mitume sio kama alibahatisha ila tayar walikwisha pangwa kutumika, ndio maana kwenye Yohana 17:12 ?,NILIPOKUWAPO PAMOJA NAO,  MIMI NALIWALINDA KWAJINALAKO ULILONIPA, NIKAWATUNZA;WALA HAPANA MMOJAWAPO ALIE POTEA, ILA YULE MWANA WA UPOTEVU ILI ANDIKO LITIMIE?.  tunaona akiwakabidhi kwa Mungu kama Baba alivyo mpa awajenge yeye akiwa kama mchungaji na mfano kwao nao wakatende kama yeye,

Kwahiyo mpendwa ili Yesu leo afanye kazi yake anakuhitaji wewe,

YESU AMEKUITA ILI UMTUMIKIE,
Somo na Mtumishi Shio Expery.

Thursday, 25 February 2016

ALHAMISI WIKI YA 2 YA KWARESMA





Somo: Yer 17:5-10  Zab: 2:1 1-2, 3-4, 6  Injili: Lk 16:19-31

Nukuu:

Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana,? Yer 17:5

Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake,? Yer 17:7

Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake,? Yer 17:10

Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.? Lk 16:29,31

TAFAKARI:
Kuishi bila hofu ya Mungu; kutotimiza wajibu na kutokujali.?

Wapendwa wana wa Mungu, niwaalike tena kwa siku ya leo, tutafakari pamoja, ?kuishi bila hofu ya Mungu; kutotimiza wajibu na kutokujali.? Somo letu la kwanza laelezea hathari za kuishi bila kuwa na hofu ya Mungu. Injili yatuelezea hathari za kutotimiza wajibu na kutokujali.

Ndugu, tuanze safari yetu kwa kutafakari kwa undani hathari za kutokuwa na hofu yangu. Je, hofu ya Mungu ni nini? Mpendwa, hofu ya Mungu ni kuishi kwa kumtegemea Mungu kwa kila jambo. ?
Ee Bwana, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki,? Zab 40:5.

Ni kujenga mahusiano ya karibu na Mungu kiasi kwamba huwezi fanya lolote bila kumshirikisha Mungu. Ndugu yangu, ?mkabidhi Bwana kazi zako, na mawazo yako yatathibitika,? Mit 16:3. Mtu anayeishi katika hofu ya Mungu, upanga na Mungu, uwaza na Mungu, ushauriana na Mungu, na uyakabidhi maisha yake mwenyewe na mipango yake yote kwa Mungu. Huku ni kuishi katika baraka kama asemavyo Nabii Yeremia, ?Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake,? Yer 17:7

Kuishi bila hofu ya Mungu ni kujiamini kusiko fikirika. Ni kuamini na kutegemea vitu na mali, watu na vyeo vyao. Huku ndiko tunapochuma laana kama anavyosema Nabii Yeremia, ?Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana,? Yer 17:5. Mtu wa mwono huu kimaisha hawezi pata baraka. Mungu hana nafasi katika maisha yake. Na hapendi kumpa Mungu nafasi.

Mtu asiye na hofu ya Mungu huishi maisha linganishi mara zote. Mtu wa mtindo huu kimaisha hawezi jipokea alivyo; na hivyo ni vigumu kufanya mabadiliko kimwili na kiroho. Mtu wa mtindo huu awezi kuwa na furaha ya kweli. Muda wote huishi maisha ya ushindani na kusahau jambo lililo la msingi katika maisha yake, yaani, Mungu hupendezwa nawe kama ulivyo. Uwepo wake ulimwenguni hapa si bahati mbaya. Maisha bila Mungu ni sawa na samaki bila maji. Hivyo ni wajibu wangu na wako kuitafuta sura ya Mungu kila siku.?
Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako,? Zab 17:15. Kwa nini basi itakupasa kuitafuta sura ya Mungu kila siku? Mtume Paulo anasema,?
Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni,? 1Kor 15:49. Na sura ya yule wa mbinguni ni UTAKATIFU. Ndugu yangu, bila Utakatifu hakuna mbingu. Kuitafuta Sura ya Mungu ni kuutafuta Utakatifu na kuuishi huo utakatifu tungali hai kila mmoja wetu kadiri ya mazingira na wito wake.

Furaha ya kweli haipatikani kwa mali tulizonazo; bali twaipata kwa kujipokea kama tulivyo na kujua upendo wa Mungu ndani yetu. Yeye Mungu yupo tayari kutupokea na kutufanya tena wana wake tunapokiri kupotoka kwetu na kumuasi. Mungu huturudishia hadhi yetu na mastahili yetu kama watoto wake. Hii ndiyo furaha ya kweli ndani mwetu. Hakuna mamlaka yoyote au binadamu yeyote awezaye kuyafanya haya. Ni Mungu tu.

Somo la Injili la tupa kisa cha tajiri na maskini Lazaro. Tajiri anajulikana kwa mwono wake, na maisha yake ya anasa. Lazaro anajulikana kwa jina lake, umaskini wake na unyonge wake. Kosa kubwa la tajiri huyu ni dhambi ya kutotimiza wajibu. Ndugu yangu, kabla ya kuendelea na tafakari hii nikuombe usali kwanza sala ya ?NAKUUNGAMIA.? Dhambi ya kutotimiza wajibu, ni kosa la nne tunalokiri katika sala hii ya ?nakuungamia Mungu mwenyezi.? Lazaro tunaambiwa mara zote alikaa kwenye mlango, ikimaanisha kwamba kwa vyovyote vile tajiri huyu alimwona Lazaro katika dhiki yake na ilimpasa tajiri huyu afanye kitu. Kutotimiza wajibu, ni kosa la kutokufanya kitu wakati ulitakiwa kufanya kitu. Tajiri huyu anahukumiwa kwa kutokujali na kutokufanya chochote.

Ndugu yangu, tazama mazingira unayoishi, Je, akina Lazaro hawapo? Wale Mungu aliotubariki kuwa na Magari binafsi, Je, unapofunguliwa geti hujamwona Lazaro pembeni akisubiri wema na upendo wako? Wale ambao hula vizuri kila siku na asubuhi kumwaga viporo vya wali na vipande ya samaki, Je, huwaoni akina Lazaro wakilichungulia shimo taka kwa masikitika? Wewe ambaye kila siku huingia ofisini na mkoba wako, Je, humuoni Lazaro kwenye benchi akisubiri wema na huruma yako?

Ukweli ni kwamba, wote tutakufa na kujongea kiti cha ukumu. Tunapoishi hapa duniani, tunaaswa na mzaburi, ?usiogope mtu atakapopata utajiri, na fahari ya nyumba yake itakapozidi. Maana atakapokufa hatachukua cho chote; utukufu wake hautashuka ukimfuata,? Zab 49:16-17. Mambo yote yatupayo ufahari ipo siku tutayaacha. Je mbele ya Mungu tutafika na jambo gani kama utambulisho wetu?

Ndugu yangu, ijumaa ijayo, nakualika wakati wa njia ya msalaba utafakari kituo cha tisa; Yesu anaanguka mara ya tatu. Njia ya msalaba kwa kutumia misale ya waamini, kuna maneno haya katika kituo hiki cha tisa; ?Mara nyingi mno ninajibovusha kwa kupenda mno starehe, anasa na tafrija. Ee Yesu mwema, nisaidie kuufuata mfano wa Mtakatifu Paulo, niutese mwili wangu na kuutumikisha, ili nipate siku moja tuzo mbinguni.? Katika kujibovusha huko, hujakutana na akina Lazaro?

Tunapojitesa na kuwajali wengine, hakika tutapata tuzo mbinguni. Mateso aliyoyapata Tajiri, alitamani na kuomba taarifa zile ziwafikie ndugu zake ili wasije patwa na mateso yale. Ibrahimu anamjibu, ?Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.? Lk 16:29,31. Ndugu yangu, hapa Musa anawakilisha Sheri za Mungu na Amri zake. Manabii hapa ni wale wahudumu wa neno la Mungu. Kwa maana nyingine tungesema, sisi kama wafuasi wa Kristo tunajua taratibu zitupasazo kuishi, ikiwa ni pamoja na Amri za Mungu. Na Amri kuu kupita zote ni Amri ya upendo.?
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii,? Mt 22:37-40 Pili, tumepewa wachungani, na wapo muda wote kwa kutuhudumia hasa kiroho. Tunaonywa na kufundishwa kupitia mahubiri yao. Kwa kuyashika haya mawili na kuyaishi, basi tuzo tutalipata. Nje ya hapo tutegemee mateso makali.