Zaburi 42:1

Kama paa atamanivyo maji ya kijito,ndivyo ninavyokutamani ee Mungu wangu...!!.

Zaburi 42:2

Naona kiu ya Mungu,kiu ya Mungu alie hai,nitafika lini kwake na kuuona uso wake..?.

Zaburi 42:3

Machozi yamekuwa chakula changu mchana na usiku,waliponiambiakila siku 'yuko wapi Mungu wako?'.

43:4

Nakumbuka tena mambo haya kwa majonzi moyoni mwangu:Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu,nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Mungu wakipiga vigelegele vya shukrani;umati wa watu wakifanya sherehe!.

Zaburi 42:5

Mbona nasononeka hivyo moyoni? Kwa nini nahangaika hivyo ndani mwangu? Nitamtumainia Mungu, maana nitamsifu tena yeye aliye msaada wangu na Mungu wangu

Wednesday, 9 March 2016

MUNGU WA KWELI HUJITAMBULISHA MWENYEWE

SHALOM!!!!
BWANA YESU APEWE SIFA!!!Mpendwa katka Kristo Yesu aliye Mwana wa Mungu ambaye ndio kifo chake kimetupa haki ya kwenda mbele za Mungu moja kwa moja kupitia jina lake ambalo ni zaid ya majina maana kwa Jina la Yesu lazma kila goti lipigwe!!!
Mpendwa wangu nina matumaini yakua umzima na kama ni mgonjwa pokea uponyaji kwa jina la Yesu.
Karibu tujifunze somo hili ambalo lina kichwa
MUNGU WA KWELI HUJITAMBULISHA MWENYEWE
Sehemu yoyote au mahali popote ambapo Mungu yupo na Mungu huyo ndio muumba vyote huwezi kutumia nguvu wala mapanga au silaha, maana Mungu hujitambulisha mwenyewe kwa matendo yake makuu tena na utisho mkubwa. Kiasi chakwamba hata yule ambaye alikua anaabudu Mungu mwingine tofaut na Mungu aliyeumba mbingu na Nchi lazma akili yakwamba huyu ndio Mungu wa kweli.
YONA 1:1-17
Biblia lnatufundisha habari za Mtumishi wa Mungu Yona lnaeleza kuhusu maagizo ambayo Yona alipewa kutoka kwa Mungu lakin Yona alikaidi maagizo hayo ukisoma mstr wa kwanza na wa pili Unasema Basi neno la Bwana lilimjia Yona mwana wa Amitai kusema,(2) Ondoka uende Ninawi mji ule mkubwa ukapige kelele juu yake kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
Lengo la Mungu alitaka Yona aende ule mji akahubiri habari njema za Mungu ili watu wa ninawi watubu nakuacha njia zao mbaya wapate kumrudia Mungu lakin Yona alitowa hukumu ndani ya moyo wake kwa maana hakutaka waninawi wasamehewe kwa maana maovu yao yalikua makubwa.
Ndipo Yona akaondoka kuelekea Tashrshi ili kujiepusha na Bwana lakin Mungu hakutaka kumwacha Yona naye aende alimfuata mpaka alikokua anaelekea mstr wa, (4) Unasema Lakin Bwana alituma upepo mkuu Baharin lkawa tufani kubwa baharini, hata merikebu lkawa karibu kuvunjika mstr 5) ambao ndio point yetu ya msingi unasema, basi wale mabaharia wakaogopa kila mtu akamwomba mungu wake nao wakatupa baharini shehena iliyojua merikebuni ili kupunguza uzito wake lakin Yona alikua ameshuka pande za ndani ya merikebu akajilaza akapata usingizi .


Kwenye mistr hii miwiri hasa mstr wa (5) Unasema Basi mabaharia wakaogopa kila mmoja akamwomba mungu wake,- Katka mstr huu tunaona kwamba kila baharia alikua na Mungu wake na kila mmoja alimwomba huyo Mungu lakin tufani haikutulia Kwa maana Mungu wa Yona ambaye ndiio Mungu mkuu ndio aliyechafua bahari. Na Yona kwakujua hayo kwamba tufani ni kwa ajili yake alienda pande za chini na kuuchapa usingizi bila waswas wowote. Mpendwa huenda na wewe ndio cha matatizo katka familia yako kwa maana umekimbia kazi ya Mungu nakushauri rudi umpokeye Yesu. Lakin katika yote Yona alipouliza alikubali kwamba tufani ni kwa ajiri yake naye akachaguwa wamtupe baharin. Mstr wa 13 unaonyesha mabaharia wakimlilia Bwana na hapa ni baada ya kugundua kua yupo Mungu mkuu zaid ya miungu waliokua wakiabudu na kuiomba kabla ya tufani, mstr wa 15 unasema basi wakamkamata Yona nakumtupa baharini nayo bahari lkaacha kuchafuka mstr wa 16 ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno wakamtolea Bwana sadaka na nadhiri
Watu hawa ambao ni mabaria waligundua uwepo wa Mungu ambaye nimuweza wa yote baada ya kuona matendo makuu na pale pale walikiri nakuanza kumwomba na baada ya kumtupa Yona baharin na bahari kunyamaza ndipo wakaogopa tena wakamtolea Bwana sadaka na kuweka nadhiri. Mpendwa ninakuambia katka jina la Yesu yakwamba MUNGU HUJITAMBULISHA MWENYEWE.
>>> Nakukaribisha katka huduma ya Maombi Nyumbani kwa Mzee Magongo Kinondoni Mkwajuni. Tunatazamana na nyumba ya Diwani Mhe Kimbita. Njoo tumuombe Mungu kwa pamoja naye atakufungua naye atajidhihirisha kwako kama alivyojidhirihidha kwa mabaharia, kupitia neno lake pamoja na maombi. Kwa mawasiliano zaidi tuma msg au piga +255656995917 Goba unashuka kituo cha Contena halaf piga cmu.
>> Mungu akubariki sana Amen<<




Friday, 4 March 2016

KUSONGA MBELE LAZIMA.








SHALOM!!!
Ninamshukulu Mungu aliyeumba mbingu na nchi kwakua ameifanya siku ya leo, Naye ameniamsha vyema kabsa, Sifa na utukufu ni kwako Bwana Mungu wa majeshi uliye muweza wa yote Amen.
Mpendwa katka Kristo Yesu karibu Tujifunze jambo kwakua sote tumefanyika wanafunzi wa Yesu.


Yamkini upo katka hali ambayo bado hujapata majibu yakwamba mwisho wake nin juu ya jambo ambalo linakutatiza. Katka maisha kuna mapito mengi, majaribu nayo nimengi, lakin kwa jina la Yesu ninakwambia
KUSONGA MBELE LAZIMA
huenda usielewe kwanini ninasema kusonga mbele lazma, lakin nikwakua wewe sio wa kwanza kupitia magumu, mapito na majaribu unayopitia, walikuwepo watu walipitia magumu na mateso mengi lakin kwa msaada wa Bwana waliweza kushinda. Hata kama ni vita ya kiroho lazma ujuwe kwamba ni mpila peke na michezo mingine ndio wanaweza kupata droo kwa maana ya kutofungana, au kufungana magoli yaliyo sawa, lakin vita ya kiroho lazma awepo mshindi na siku zote Elishadai Jehova ndio Mungu asiye shindwa. Haleluyaaaaaa!!!!!
Biblia katka kitabu cha Kutoka 14:11-16 lnatueleza habar za wana wa lsrael na jeshi la Farao, wana wa lsrael waliona bahari ya shamu mbele yao, Nao walikata tama walijua mwisho wao umefika, Ndipo wakanung'unika mbele ya Musa. Wakasema mstr wa 11 Kwasababu hapakua na makaburi katka Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mpendwa nawe huenda unajiuliza maswali mengi juu ya hatma yako, huenda umefika wakat unasema Mungu amekuacha lakin lipo neno la matumaini kwako bado kwa maana Mungu hajakuacha. Mstr wa 13  Musa anawambia
Msiogope simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele (14)  Bwana atawapigania ninyi nanyi mtanyamaza kimya. Jina la Bwana libarikiwe sana
Mpendwa katka Kristo Yesu Musa wakat anasema maneno haya yeye mwenyewe hakujua Mungu atawaokowa vip na ataanzia wap? Lakin yeye alimwamini Mungu kwamaana alijua safari yao lmepangwa na Mungu. Nami nakueleza yakwamba huenda hujui na huelewi yakwamba Mungu atakupigania vip na ataanzia wap lakin yeye ni Bwana wa majeshi naye ni mshindi!!! Sema Amina! Kubwa!!! Licha ya Musa kusema kwa ujasiri lakin hakujua ni wapi nayeye anziye na ndio maana mstr wa (15) Mungu anamwambia Musa Bwana akamwambia Musa mbona wanililia mim? Wambie wana wa lsraeli waendelee mbele. Hoo haleluya Mungu anamwambia Musa kwa nin unanililia? Kumbe Musa naye wakat anasema maneno yale alikua akilia ndani ya moyo wake lakin kilikua nikilio cha kumwomba Bwana na sio kilio cha kunung'unika kama wana wa lsraeli walivyolia Musa alikuwa akisema tusaidie Bwana usituache!! Lakin alisahau yakwamba anayo fimbo mkononi mwake. Lakin cha ajabu Mungu anamwambia Musa wambie wana wa lsraeli WAENDELEE MBELE, YANI WASONGE MBELE. sio kwamba Mungu hakuiona bahari aliona lakin anasema WAENDELEE MBELE. KUSONGA MBELE nami kwa jina la Yesu Kristo wa nazaret aliyekufa kwa ajili yako na yakwangu nakwambia lazma usonge mbele hata kama mbele kuna bahari hata kama huna matumaini, hata unaona ukuta lakin Kusonga mbele lazma. Kwa maana yupo Bwana wa Majeshi naye anayaona unayopitia naye atatenda mambo makubwa juu yako nawe utanyamaza kimya. Musa anaambiwa lnua fimbo yako, ukanyoshe mkono waki juu ya bahari na kuigawanya nao wana wa lsraeli watapita kati ya bahari katka nchi kavu. Mungu alitenda muujiza mkubwa ambao wana wa lsraeli hawakutegemea nami nakushauri endelea kuomba endelea kuomba wala usichoke maana upo muujiza mkubwa mbele yako. Biblia lnasema katka kitabu cha
Isaya 40:28-31Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, Bwana, muumba miisho ya dunia, hazimii wala hachoki akili zake hazichunguziki 29 Huwapa nguvu wazimiao humwongeza nguvu yeye asiye na uwezo. Akili za Mungu hazichunguziki Dada yangu, kaka yangu, Mama yangu mdogo wangu kwa maana wakat wewe unaona bahari kama wana wa lsraeli yeye anaona nchi kavu ndani ya bahari.KUSONGA MBELE LAZMA  NDUGU kwa maana lipo neno la matumaini kutoka katka kitabu cha
Isaya 43:1-3  Umeitwa kwa jina lako upitapo katka maji mengi nitakuwa pamoja nawe, na katka mito haitakugharikisha uendapo katka moto hauteketea wala mwali wa moto hautakuunguza. Hoo!!Haleluya!!!!! Maana yeye ni Bwana Mungu wako ninakwambia kusonga mbele lazma na ni marufuku kukata tama. Kwa maana Bwana anakupa uhakika wakukutetea. Ubarikiwe sana.
By Samuel M Mendulo
Samendulo@gmail.com.
Namba +255656995917 Amen

Juma la 3 la kwaresma


Alhamisi 3 2016
Somo la 1
Yer. 7:23-28

Naliwaamuru neno hili, nikisema, Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu; mkaende katika njia ile yote nitakayowaamuru, mpate kufanikiwa. Lakini hawakusikiliza, wala kutega sikio lao, bali walikwenda kw amashauri yao wenyewe, na kwa ushupavu wa mioyo yao mibaya, wakaenda nyuma wala si mbele. Tokea siku ile baba zenu walipotoka katika nchi ya Misri hata leo, nimewatuma watumishi wangu wote manabii kwenu ninyi, nikiamka mapema kila siku na kuwatuma. Lakini hawakunisikiliza, wala kutega sikio lao; bali walifanya shingo yao kuwa ngumu; walitenda mabaya kuliko baba zao. Nawe utawaambia maneno hayo yote; lakini hawatakusikiliza; nawe utawaita; lakini hawatakuitikia. Nawe utawaambia, Taifa hili ndilo lisilosikiliza sauti ya Bwana, Mungu wao, wala kupokea mafundisho; uaminifu umepotea, umekatiliwa mbali vinywa vyao,

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 95:1-2, 6-9 (K) 7

(K) Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu.

Njoni, tumwimbie Bwana,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi. (K)

Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake. (K)

Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Msifanye migumu mioyo yenu;
Kama vile huko Meriba,
Kama siku ya Masa jangwani.
Hapo waliponijaribu baba zenu,
Wakanipima, wakayaona matendo yangu. (K)

SHANGILIO
Zab. 51:10, 12

Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Unirudishie furaha ya wokovu wako.

INJILI
Lk. 11:14-23

Yesu alikuwa akitoa pepo bubu; ikawa pepo alipotoka, yule bubu akanena, makutano wakastaajabu. Wengine wao wakasema, Atoa pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo. Wengine walimjaribu, wakitaka ishara itokayo mbinguni. Naye akajua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka. Basi, ikiwa Shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli, wana wenu je! Huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo, hao ndio watakaowahukumu. Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang?anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.
Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya.

Wednesday, 2 March 2016

BADHI YA DALILI ZA KUA NA JINI MAHABA AU KASHKASH NDAN YA MWILI WA MWANADAMU

Bwana Yesu apewe sifa wapendwa!!!

1)  kuwashwa washwa mwilini kama vitu vinakutembea tembea
2) kuwaka tama sana ya ngono pindi unapokua peke yako lakin unapokua na mweza wako hamu hutoweka. Mwanaume hupoteza nguvu.
3) kuhisi au kuota unalala na mtu kitandani
4) Mwili kusisimuka mara kwa mara hasa sehemu kuanzia kiunoni kushuka chini.
5) Kutamani kua na mweza wako pindi anapokua mbali lakin akiwa karibu humchukia bila sababu za msingi.
6) Kua na hasra sana bila hata sababu za msingi
7) Kuwa na hali ya kutojali au kuthaminni wengine umimi na kujiona wa thamani peke yako kuliko wengine.
8) Kuchukiwa na ndugu jamaa na marafiki anakufanya ufanye mambo yakuchukiza wengine
9) Kujiona mtu mwenye mikosi nuksi na balaa tupu
10) Kuvurugika kwa mipango/ mambo yako/ hasa ya maendeleo na kila unachopanga hushindikana hata kama ukisaidiwa na mwisho hujiona hufai
11) Kuumwa kichwa pindi wakat unasoma Biblia au masomo ya kawaida
12) Kutokujisikia kuomba au kusinzia pindi unapotaka kuanza maombi, huishiwa nguvu kabisa, Na kuishia kuhangaika kama mtu asiyejua lakufanya
13) Kuota lbada zisizoeleweka
14) Kuota ndoto za kutisha kama unafukuzwa na watu, Mnyama , Nyoka au kuota unaanguka kwenye shimo lefu lakin hufiki chini, Mafuriko ya maji mengi na wakat mwingine maji haya huwa machafu na ndani yake kua na nyoka
15) Kuota upo kando kando ya bahari, katka mto, au porini, Sherehe za harusi, harusi au ya mtu usiyemjua lla mnakula
16) kuota una mimba au unajifungua, una mtoto
17) Kujisikia umechoka masaa yote, na kutamani kulala masaa yote kutokujisikia kufanya chochote. Kuhisi uzito wa mwili kama umebeba kitu kizito
17)  Maumivu chini ya kitovu kwa akina mama au katka mji wa uzazi
18) Kusikia maumivu makari wakat wa tendo la ndoa kwa akina mama
19) Kujihisi unaingiliwa na mwanaume au unalala na mwanamke mara kwa mara
20) Mimba kuharibika bila sababu za msingi, Kufunga hedhi bila sababu. Hizi tu ni badhi ya dalili za kuwepo jini mahaba ndani ya mwanadamu, sio lazma uwe nazo zote hapana, lakin pia sio hizi peke yake zipo nyingi sana. Na ndio maana Biblia lnatuhimiza kuulinda moyo kuliko kito chochote kile Mithali 23:26. Ukishindwa kuulinda moyo wako nirahisi sana kutawaliwa na jini Mahaba au kashikashi, na madhara yakutawaliwa na viumbe hawa ni makubwa sana. Itaendelea  kichwa NAMNA YA KUMFUNGUA MWENYE PEPO MAHABA AU KASHIKASHI.
Samuel M Mendulo
Samendulo@gmail.com
Namba +255656995917