Shalom!! Neema na lwe kwako, na rehema na aman, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana na mwokozi wetu Amen.
LUKA 19:1-10
BWANA YESU APEWE SIFA!!!
Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake, na tazama palikua na mtu jina lake Zakayo mkubwa mmoja katika watoza Ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikua akitafuta kumuona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwasababu ya umati wa watu maana ni mfupi wa kimo.....!
Mpendwa katka Kristo Yesu, biblia inaeleza kuhusu habari za mtu mmoja jina lake Zakayo naye alikua mtoza ushuru hii ni kazi ambayo alikua anafanya. Lakin pia alikua tajiri, maana yake alikua na kila kitu haswa kuhusu mahitaji ya kimwili, alikuwa amejitosheleza. Lakin mtoza ushuru huyu na tajiri alitaka kumuona Yesu ni mtu wa namna gani, huyu hakua na maombi wala mahitaji kwa Yesu bali alitaka kumuona ni mtu wa namna gani kwamaana alipata habari zake,
Bwana Yesu apewe sifa..!! Mstr wa 4 Akatangulia mbio akapanda juu ya mkuyu apate kumwona kwa kua atakuja kupitia njia ile. Zakayo alitaka kumwona Yesu lakin kukawa na kikwazo umati wa watu ulikua mkubwa sana naye alikua mfupi wa kimo, alijua kama sijatafuta njia nyingine mim Yesu sitamwona, akaumiza kichwa kufikiri afanyeje lakin mwisho akapata jibu akaona apande kwenye mkuyu. Biblia lnasema akatangulia mbio akapanda juu ya mkuyu, maana yake alikimbia ili kuwai kabla watu hawajafika eneo la mti lakin pia kwakua nimfupi lazima kulikua na kikwazo pia kwenye kupanda juu ya mti huenda aliomba msaada ili apandishwe, Mpendwa mim sijui nikikwazo kinakukwamisha ili kumuona Yesu Kristo lakin hapa tunaona jinsi ambavyo Zakayo alikabiliana na kikwazo chake, kama huwez kupanda kwenye mtii je! Umeomba watu wakupandishe? Kwa maana Zakayo alipopata jibu la kukabiliana na kikwazo cha ufupi wa kimo alikutana na kikwazo cha jinsi yakupanda kwenye mti bila shaka unajua watu wafupi wanavyopata shida kupanda mahali ambapo ni palefu. Je! Wewe na mim tumekwama wapi? Mstr wa 5 Na Yesu alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambiah Zakayo shuka upesi kwakua leo lmenipaswa kushinda nyumbani mwako HALELUYAAAA! Zakayo aliangaika kumtafuta Yesu ili amuone akatumia mbinu mbadala kumbe wakat anahangaika Yesu naye alikua anamtafuta. Ninakwambia kwa jina la Yesu kristo Kristo kuhangaika kwako sio bure kwamaana huyo Yesu naye yupo njian haijalishe unapita kwenye mazingira gan kwa maana hata Zakayo alipitia vikwazo lakin aling'ang'ana na mwisho alifanikisha ndoto yake na sio kufanikisha kumuona tu alipata nafasi ya Yesu kuingia nyumbani mwake. Biblia lnasema akafanya haraka akashuka akamkaribisha kwa furaha! Mstr wa 7 unasema hata watu walipoona walinung'unika wote wakisema ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi, huenda na wewe unakutana na mambo kama haya watu wanadai wewe ni mwenye dhambi lakin angalia baada ya Yesu kuingia nyumban mwa Zakayo maisha ya Zakayo yalibadilika ghafla Zakayo alijitambua kwamba matendo mengi ni kinyume na Yesu naye akasema mstr wa 8 Zakayo akasmama akamwambia Bwana, Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskin na lkiwa nimemnyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne, Toba safi kabisa maisha ya Zakayo yalibadilika baada ya kumtafuta Yesu kwabidii na kumuona. Mstr wa nane Zakayo anaomba toba tena anaambatanisha na sadaka ambayo ni nusu ya mali yake, lakkn haishii hpo anarudisha vitu alivyokua ananyang'anya kwa hila wakat anatoza ushuru, lakin hayo yote nibaada ya Zakayo kukabiliana na vikwazo vingi, Wewe na mim ndio Zakayo wa leo tunapitia magumu mengi katika kumtafuta huyu Yesu vikwazo ni vingi saa nyingine afadhari ya Zakayo maana yeye allikua tajiri lakin lipo tumaini kubwa juu yetu mpendwa kwamaana kuhangaika kwetu sio bure naye Yesu yu karibu atakutowa katka hiyo hali nawe utang'aa kama nyota gizan kwa maana Yesu alipoingia nyumbani mwa Zakayo alibadili maisha yake! Na mstr wa 9 Yesu anasema leo Wokovu umefika nyumbani humu kwa sababu huyu nae ni mwana wa lbrahimu. Mstr wa 10 anamaliza kwakusema kwakua Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Ni maombi yangu kwako Uendeleye kumtafuta huyu Yesu kwamaana ninao uhakika yakwamba atajibu kile kilio chako hata kama utaona anachelewa lakin wewe endeleya kumuita na kumtafuta tena kwa bidii kikwazo kisikufanye wewe kuishia njian bali pigana mpaka kieleweke.
Ubarikiwe sana
Ameeen!!!!
Monday, 15 February 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment