Friday, 26 February 2016

YESU ANAKUITA



Mwito wa Yesu ,(wito nikitendo cha kumsikia Mungu akitoa majukumu ya Utumishi wako)

Hadi unaitwa ujue ulikuwa kwenye mpango wa Mungu tangu hujazaliwa.

YEREMIA 1:5  Mungu ana sema , ?KABLA SIJA KUUMBA KATIKA TUMBO NALIKUJUA, NA KABLA HUJATOKA TUMBONI, NALIKUTAKASA; NIMEKUWEKA KUWA NABII WA MATAIFA. ?

Sasa basi hilineno lililomjja Yeremia lilikuwa ndiyo Yesu ( Neno=Yesu)

YOHANE 1:1-12 Point ipo 1:1?HAPO MWANZO PALIKUWEPO NENO,  NAYE NENO ALIKUWAKO KWA MUNGU, NAE NENO ALIKUWA MUNGU. ?

Hata leo Yesu anatuita tutende kazi yake yaani tutende mapenzi ya Baba.

YOHANA 6:38 Yesu anasema ?KWAKUWA MIMI SIKUSHUKA TOKA MBINGUNI ILI NIFANYE MAPENZI YANGU, BALI MAPENZI YAKE ALIE NIPELEKA.

Kama yeye amekuja kutimiza mapenzi ya Baba,  basi ni dhahiri kuwa anataka na wewe uyatimize vivyo hivyo,  yaani utumike kutimiza mapenzi ya Baba ila kupitia yeye.?

Mwitohuu hauchagui hali wala mali, bali yeyote atakaetii sauti hiyo, ZABURI 95:8 ?
MSIFANYE MIGUMU MIOYO YENU KAMA HUKO MERIBA KAMA SIKU YA MUSA JANGWANI,? mkisikia sauti ya Roho mtakatifu WAEBRANIA 3:7-8 ?KWAHIYO KAMA ANENAVYO ROHO MTAKATIFU, LEO KAMA MTAISIKIA SAUTI YAKE, MSIFANYE MIGUMU MIOYO YENU, KAMA WAKATI WA KUKASIRISHA , SIKU YA KUJARIBIWA KATIKA JANGWA,?

kumbuka Dhumuni kubwa ni wewe kutumika ili kazi ya Mungu ifanyike kupitia wewe YEREMIA 51:20-23, nitakuonesha mstar wa 20,?WEW U TLRUNGU LANGU NA SILAHA ZANGU ZA VITA,  KWA WEWE NITAVUNJA VUNJA MATAIFA ,  NA KWA WEWE NITAHARIBU FALME. ?

Katika wito huu pia Mungu anatuhakikishia usalama katika kutenda kazi nae ! YOSHUA 1:9 ?
JE!  SI MIMI NILIE KUAMURU?  UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA;USIOGOPE WALA USIFADHAIKE;KWAKUWA BWANA MUNGU WAKO,  YU PAMOJA NAWE KILA UENDAKO. ?

Nakila silaha ya kufanya kazi tunayo, 2PETRO 1:3 ?KWAKUWA UWEZA WAKE WA UUNGU UMETUKIRIMIA VITIVYOTE VIPASAVYO UZIMA NA UTAUWA, KWAKUMJUA YEYE ALIETUITA KWA UTUKUFUWAKE NA WEMA WAKE MWENYEWE?, Kwahiyo tunakila sababu ya kutii,  Yeremia alisema YEREMIA 1:6  ?NDIPO NILIPOSEMA, AA,  BWANA MUNGU! TAZAMA SIWEZIKUSEMA MAANA MIMI NI MTOTO?. na Mungu akamjibu YEREMIA 1:7-87-8 ?LAKINI BWANA AKANIAMBIA USISEME, MIMI NIMTOTO;MAANA UTAKWENDA KWA KILAMTU NITAKAE KUTUMA KWAKE, NAWE UTASEMA KILA NENO NITAKALO KUAMURU, USIOGOPE KWA SABABU YA HAO MAANA MIMI NIPO PAMOJA NAWE NIKUOKOE, ASEMA BWANA.?

Tujifunze kukubali wito na tusali sala ya kushukuru na kupokea ule wito tulio itiwa. Marium alipewa wito wa kuchukua mimba na kumzaa Yesu ambae leo nimkombozi wetu,  katika mwito ule yeye  ali uitikia na kuupokea kikamilifu,  LUKA 1:38 ?MARIUM AKASEMA ,  TAZAMA MIMI NI MJAKAZI WA BWANA NAIWEKWANGU KAMA ULIVYOSEMA . KISHA MALAIKA AKAONDOKA AKAENDA ZAKE.?  lakini tukirudi nyuma kidogo LUKA 1:26-37.  Utaona Marium aliuliza masali ili kufahamu wito wake kisawasawa,  hata wewe waweza kusali na kumuuliza Mungu ili akufunulie na kukufanya uujue,   Waefeso 1:17-23 point ipo kwenye 18, ?
MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU, MJUE TUMAINI LA MWITO WAKE JINSI LILIVYO, NAUTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHIWAKE KATIKA WATAKATIFU  JINSI ULIVYO?

Sasa basi Yesu anatuita kwenye wito ili tujenge kanisa ambalo yeye mwenye ndio kichwa cha kanisa lenyewe, WAKOLOSAI 1:18 ?
NAE NDIO KICHWA CHA MWILI YAANI CHA KANISA,NAYE NI MWANZO , NI MZALIWA WA KWANZA KATIKA WAFU, ILIKWAMBA AWE MTANGULIZI KATIKA YOTE. ?

Yesu alipotoka jangwani kujaribiwa alianza kwa kuwaita wale mitume Mathayo 4:18-21 ,  ambao waliongozana nae katika kutenda kazi, kazi yao kubwa ilikuwa kufanya kazi na Yesu pamoja na kujifunza kumjua Mungu kupitia Yesu,

Nahawa aliowateuwa kuwa mitume sio kama alibahatisha ila tayar walikwisha pangwa kutumika, ndio maana kwenye Yohana 17:12 ?,NILIPOKUWAPO PAMOJA NAO,  MIMI NALIWALINDA KWAJINALAKO ULILONIPA, NIKAWATUNZA;WALA HAPANA MMOJAWAPO ALIE POTEA, ILA YULE MWANA WA UPOTEVU ILI ANDIKO LITIMIE?.  tunaona akiwakabidhi kwa Mungu kama Baba alivyo mpa awajenge yeye akiwa kama mchungaji na mfano kwao nao wakatende kama yeye,

Kwahiyo mpendwa ili Yesu leo afanye kazi yake anakuhitaji wewe,

YESU AMEKUITA ILI UMTUMIKIE,
Somo na Mtumishi Shio Expery.

0 comments:

Post a Comment