
Yohana 17:1-10
Maana ya uzima= Nihali ya kuwa na afya njema.
Maana ya Milele= Ni bila kua na mwisho.
Lazima kujua kua mtu anaanza kuishi maisha ya uzima akiwa dunian, ili kutengeneza maisha ya uzima wa milele nilazima huyu mtu awe nao uzima wa kimwili ambao ni maisha ya dunian. Lakin ukweli nikwamba maisha ya uzima wa milele yanaanzia dunian. Neno uzima wa milele linamaana pia ya Maisha baada ya kifo. Wokovu upo duniani kwa njia ya Yesu kristo baada ya kufa ni hukumu. Nimekua nikisikia wachungaji wakiomba kwa namna yaajabu ambayo sikupata kuelewa. Wengine wakisema sadaka ambayo wametowa watu wakat wa lbada ya mazishi lmtakase marehemu ili apate kusamehewa dhambi, lakin huu ni uongo ambao hauna mantiki yoyote kwa maana mtu anapokufa kinachofuata nikusubiri hukumu, Usije ukaamini hata siku moja kwamba maombi yako yanaweza kubadilisha hali ya marehemu akawa msafi hapo utakua unajidanganya. Au ukawa na wazo kwamba usipookoka na kuishi maisha matakatifu basi ukifa mchungaji, au mtumishi wa Mungu akikuombea wewe utatakasika nakupata uzima wa milele hiyo nayo ni ndoto ya mchana. Wakat wakutengeneza maisha ya baadae kwa maana ya maisha baada ya kifo ni sasa au msisha ya uzima wa milele, Kwa maana biblia lnasema Wokovu ni sasa hivyo lazma kuokoka na kudumu katka maisha ya kumpendeza Mungu kama unania ya kupata uzima wa milele.
Yohana 10:14-17
Mstr wa (10) Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu, Mim nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele
Neno hili mpendwa linatupa uhakika yakwamba Yesu alikuja ili tuwe na uzima kwa maana ya afya njema. Mwivi ni shetani ambaye analeta magonjwa kinyume na mpango wa Yesu wakutupa uzima tena sio uzimatu bali uzima tele. Kwasababu biblia lnasema lli litimie lile neno lililonenwa na nabii lsaya akisema
Mwenyewe aliutwa udhaifu wetu, Na kuyachukua Magonjwa yetu Mathayo 8:17 Maana yake nikwamba ukiwa ndani ya Kristo Yesu ni marufuku kuumwaumwa kwamaana aliyachukua magonjwa yetu nayo yakawa ya kwake na kwa kupigwa kwake tumepona. Hii ndio maana ya uzima kwa maana ya afya njema. Tatizo tulilokua nalo pale magonjwa yanapokuja tunakimbilia kufadhaika na kulalamika lakin magonjwa ni mpango wa shetan kwa ajili ya kuwatesa wana wa Mungu lakin jambo hili Mungu alilijua mapema na ndio maana maandiko yako wazi. Kama unaumwa umapaswa kutumia vifungu kama hivi kudai hali yako ya uzima na Mungu lazma atakuponya kwamaana yeye hapinngani na neno lake, unapodai lazima alitimize lakin kudai huku nilazma pia uwe nayo haki kwa maana ya matendo mema maana Mungu hasikilizi maombi ya mwenye dhambi, hivyo kabla yakudai haki lazma ufanye toba kwamaana ya kujitakasa.
UZIMA WA MILELE
Kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliyompa awape uzima wa milele
Mstr huu unatuonyesha yakwamba Mungu alimpa Yesu mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili awape uzma wa milele, maana yake uzima wa milele unaishi ndani ya Kristo Yesu. Na ndio maana unapompokea Yesu ndio chanzo cha uzima wa milele, pale ndipo unaanza kutengeneza maisha ya baada ya kifo, yan uzma wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujuwe wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. Yohana 17:1-3 Yesu ndio anatupa uzima wa milele lakin kumjua Mungu wa kweli na Yesu ambaye alitumwa kwetu ili kutupa huo uzima wa milele. Kwa njia ya msalaba. Ninakueleza kwa jina la Bwana yakwamba kumjua Mungu ndio uzma wa milele kwa maana ukimjua Mungu utaishi maisha yanayoendana na Mungu. Yohana
Biblia lnasema Twajua yakua mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi bali yeye alizaliwa na Mungu hujilinda ukisoma 1 Yohana 5:18-21 biblia lko wazi kwamba kama umeokoka huwez kutenda dhambi kwa maana unajua jinsi ya kujilinda kwasababu Huyu Yesu anakaa ndani yako. Hivyo kama unahiraji uzma wa milele lazma ujilinde na uovu. Na kama unafanya basi uache kabisa laazma ujuwe hakuna dhambi ndogo wala kubwa zote ni dhambi. Ubarikiwe sana
Somo limeandaliwa na Mtumishi Samuel M Mendulo
Samendulo@gmail.com
Namba +255656995917 Amen
0 comments:
Post a Comment