Bwana Yesu apewe sifa wapendwa!!!. UFUNUO WA YOHANA 12:7:12. Kulikua na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbingu 12 ……… Ole wa nchi na bahari kwa maana yule lbilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi akijua yakuwa ana wakati mchache, Vita hii ndio lnayoendelea juu ya malaika wa shetani ambao ndio majini, mapepo, kupitia waganga wa kienyeji na wachawi, hapa hakuna cha jini mzuri wa baya majini wote ni wabaya kwa maana walimuasi muumba wao pamoja na lusifa ambaye alikuwa malaika wa sifa huko mbinguni naye akataka kupindua selikali ya ufalme wa Mungu muumba mbingu na nchi, baada ya kushindwa akatupwa huku chini makao ya lusifa ni kuzimu na malango yake yapo baharini, kila nchi lna malango ya kuzimu.
HIZI NDIO DALILI ZA UWEPO WA JINI MAHABA NDANI YA MWANADAMU AU MAJINI AINA NYINGINE WAHARIBIFU KAMA WANAVYOTUMWA NA MAWAKALA WENGINE WACHAWI NA WAGANGA.
1) kuwashwa washwa mwilini kama vitu vinakutembea tembea
2) kuwaka tama sana ya ngono pindi unapokua peke yako lakin unapokua na mweza wako hamu hutoweka. Mwanaume hupoteza nguvu.
3) kuhisi au kuota unalala na mtu kitandani
4) Mwili kusisimuka mara kwa mara hasa sehemu kuanzia kiunoni kushuka chini.
5) Kutamani kua na mweza wako pindi anapokua mbali lakin akiwa karibu humchukia bila sababu za msingi.
6) Kua na hasra sana bila hata sababu za msingi
7) Kuwa na hali ya kutojali au kuthaminni wengine umimi na kujiona wa thamani peke yako kuliko wengine.
8) Kuchukiwa na ndugu jamaa na marafiki anakufanya ufanye mambo yakuchukiza wengine
9) Kujiona mtu mwenye mikosi nuksi na balaa tupu
10) Kuvurugika kwa mipango/ mambo yako/ hasa ya maendeleo na kila unachopanga hushindikana hata kama ukisaidiwa na mwisho hujiona hufai
11) Kuumwa kichwa pindi wakat unasoma Biblia au masomo ya kawaida
12) Kutokujisikia kuomba au kusinzia pindi unapotaka kuanza maombi, huishiwa nguvu kabisa, Na kuishia kuhangaika kama mtu asiyejua lakufanya
13) Kuota lbada zisizoeleweka
14) Kuota ndoto za kutisha kama unafukuzwa na watu, Mnyama , Nyoka au kuota unaanguka kwenye shimo lefu lakin hufiki chini, Mafuriko ya maji mengi na wakat mwingine maji haya huwa machafu na ndani yake kua na nyoka
15) Kuota upo kando kando ya bahari, katka mto, au porini, Sherehe za harusi, harusi au ya mtu usiyemjua lla mnakula
16) kuota una mimba au unajifungua, una mtoto
17) Kujisikia umechoka masaa yote, na kutamani kulala masaa yote kutokujisikia kufanya chochote. Kuhisi uzito wa mwili kama umebeba kitu kizito
17) Maumivu chini ya kitovu kwa akina mama au katka mji wa uzazi
18) Kusikia maumivu makari wakat wa tendo la ndoa kwa akina mama
19) Kujihisi unaingiliwa na mwanaume au unalala na mwanamke mara kwa mara
20) Mimba kuharibika bila sababu za msingi, Kufunga hedhi bila sababu. Hizi tu ni badhi ya dalili za kuwepo jini mahaba ndani ya mwanadamu, sio lazma uwe nazo zote hapana, lakin pia sio hizi peke yake zipo nyingi sana. Na ndio maana. LINDA SANA MOYO WAKO Biblia lnatuhimiza kuulinda moyo kuliko kito chochote kile Mithali 23:26. Ukishindwa kuulinda moyo wako nirahisi sana kutawaliwa na jini Mahaba au kashikashi, na madhara yakutawaliwa na viumbe hawa ni makubwa sana. kichwa NAMNA YA KUMFUNGUA MWENYE PEPO MAHABA AU KASHIKASHI AU AINA YOYOTE YA MAJINI. = Viumbe hawa ni viumbe wasionekana, maana yake ni roho hawaonekani kwa umbo la kibinamu japo wana uwezo wakujigeuza chochote. na mara nyingi hutumwa na wachawi, na waganga ili kumdhuru mtu au kumharibia au kumtumikisha, kwasababu ya wivu au kutafuta utajiri, lakini pia wanapokupenda wenyewe huingia ndani yako na kufanya makao, ndani yako haswa kwa wale ambao hawajaokoka, yaani kumpa Yesu maisha yako au hata kama umeokoka lakin njia zàko si njema mbele za Mungu. NJIA YA KUEPUKA MATESO YA VIUMBE HAWA NI UTAKATIFU NA IBADA, MAOMBI YA MARA KWA MARA. viumbe hawa ni mawakala shetani, Ibilisi, joka lusifa hawa ndio malaika walioasi pamoja na lusifa baada ya kupigwa mbinguni na kutupwa huku sasa wanapambana na wanadamu. ( tafakari kwa kina mistr hii) UFUNUO WA YOHANA 12:7-12. Mstr wa 7 Unasema kulikua na vita mbinguni Mikaeli na Malaika wakapigana na yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake 8 Nao hawakushinda wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Mstr 12 ………… Ole wa nchi na bahari kwa maana yule lbilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi akijua kuwa ana wakati mchache. = Hawa malaika wanaotajwa hapa kama malaika wa shetani ndio majini na mapepo nk. NAMNA YA KUOMBA ILI KUFUKUZA VIUMBE HAWA NDANI YA MWANADAMU (1)Omba toba kwa Mungu ili akusamehe dhambi zote ambazo umezifanya kwa mwili pamoja na rohoni yaani dhambi kupitia ndoto chafu, Omba toba kwa ajili ya madhara ambayo umeyata kwenye ulimwengu wa roho lkiwa kuzaa au kuzalisha watoto wa majini,kupandikizwa umasikini, roho za uzinzi na umalaya, nk Omba toba kwa ajili ya familia na ukoo kama kuna mwingilianon wowote, au kurithishwa kutoka kwenye familia na ukoo lsaya 43:25 Zaburi 51. toba ni njia ya kutafuta utakatifu mbele za Mungu aliye hai. KARIBISHA UWEPO WA MUNGU baada ya toba Mathayo 6:9-10=Unashusha ufalme wake Mungu. Unamwita Mungu kwa maana yeye anasema niite nami nitaitika Yeremia 33:1-3/6 OMBA MWONGOZO WA ROHO MTAKATIFU. Jifunike kwa damu ya Yesu funika ndugu jamaa na marafiki kazi biashara kila kitu ambacho unajua kinaweza kushambukiwa na shetani wakati unaomba au kumwombea Mtu funika kwa damu ya Yesu. Vaa silaha za Mungu Waefeso 6:11-18 maana vita hii sio ya damu na nyama bali ni katika ulimwengu wa roho juu ya falme na mamlaka juu ya wakuu wa giza yaani (Wachawi na waganga,) na majeshi yaani (majini yenyewe) na mapepo wabaya katika ulimwengu wa roho kuanzia mstr wa 13 ndio silaha zenyewe. Hakikisha una uhakika na kile unachofanya maana lmani ni hakika ya mambo ya tarajiwayo ni bayana ya mambo ya siyoonekana. Maana lngawa tunaenenda kwa mwili hatufanyi vita jinsi ya mwili, ( maana silaha za vita vyetu si vya mwili, bali zinauwezo katika Mungu hata kuangusha ngome 2 Wakorintho 10:1-6 Kwa jina la Yesu!!! anza Kuvunja mikataba na na maagano uliyoingia kwa njia ndoto, kama uliota unafunga ndoa vunja, kama uliota mjamzito na kisha kujifungua mpaka unanyonyesha vunja, peleka moto wa Yesu mwaga damu ya Yesu. Vunja mikataba yote uliyofungamanishwa nayo, na mikata hii wanaweza kukufungisha ndoa na jini chini ya bahari au njia panda au kwenye miti milefu au kwenye milima au angani, Mungu aliyeumba mbingu na nchi ni moto ulao lta moto kwa jina la Yesu Kristo vunja hiyo mikaba yote ya ndoa, Umaskin kutumikishwa nyota yako kutumika kichawi, vifungo vyote vifunguwe kwa damu Yesu kamba zote za kichawi katakata kwa upanga wa neno la Mungu maana neno la Mungu ni upanga ukatao kuwiri, Vunja kila madhabahu lnayokushikilia, lwe ya mizimu, yakichawi, yamapepo vunja Yeremia 1:9-10. Mungu amekufanya wewe kuwa kuhani na mfalme naye amekuweka juu ya falme zote ili kung' oa na kubomoa, na kuharibu na kuangamiza, ili kujenga na kupanda tena, kwa ondoa ufalme wa shetani ndani yako, familia yako ukoo wako kisha jenga ufalme wa Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu. Umepewa mamlaka ya kukanyaga joka na nge na nguvu zote za muovu shetan Luka 10:19 Achiliya moto juu ya jini Tajirini kama walitaka kukuchukua kafara,ili wapate utajiri tuma moto wa Yesu. achilia moto juu ya jini Muzafari maana huyu ndio huzuia mafanikio achiliya moto juu ya jini Anzura na Shamsu hawa ndio hufukuza wachumba nakukufunga usiowe au kuolewa, achilia moto juu ya jini Amri huyu ndio huleta ugomvi na kusababisha hasra ili kufungua mlango wa mapepo kuingia ndani yako, Funga milango yote kwa damu ya Mwana- kondoo Ufunuo 12:11, piga kwa moto ulao kama jini Tsemlee kama mimba zilikua zinaharibika hovyo,; piga moto jini Subiani kama ulikuwa huoni siku zako au zilikua zinatoka mfululizo au kidogokidogo maana huyu ndi mnywaji wa damu na husababisha ajari, piga jini Jahadi huyu ni chuma ulete anaiba pesa piga jini Latifa huyu analeta ufukura kwenye maisha, piga jini Sifariru huyu ni jini kahaba anawashawishi watu kufanya uzinzi na umalaya piga jini Maimuna kama ulikua unasikia maumivu chini ya kitovu na kuota unafanya mapenzi, WAKATI UNAFANYA HAYA YOTE USISAHAU DAMU YA MWANAKONDO MAANA MIKAELI ALISHIMNDA SHETANI KWA DAMU YA MWANA KONDOO Piga jini Ratafari kama unafuatiriwa na laana za ukoo, piga jini Janjatusi hili ndio linawafanya watu kulala usingizi wakati wa mahubiri, teketeza kwa moto ulao kila kiumbe kutoka kuzimu katika jina la Yesu vunja madhabahu zote kwa damu ya Yesu achilia damu ya Yesu lkafanyike fidia juu ya kila sadaka waliopewa majini na waganga haribu kazi zote za kishetani peleka moto kwenye malango ya kuzimu wachiye jina lako na nafsi yako, kwa jina la Yesu vunja vikao vyote vinavyokaliwa kwa ajili yako na familia. Mshukulu Mungu ukitaja majina yake kama ahsante Mungu mkombozi Mungu wa lbrahimu lsaka na yakobo, Mungu mwenye enzi, Mungu usiyeshindwa Ebeneza Jehova shalom au lmba nyimbo za sifa huku ukiamini kwamba umefunguliwa, maana neno linasema lolote mwombalo amini kuwa mmepokea nayo yatakuwa yenu, kabula ya kufanya maombi haya unaweza kufanga saa 24 au siku tatu masaa 12 kila siku ltategemea na msukumo wako, lakin kufunga sio njia ya kumshawishi Mungu kujibu maombi bali ni njia yakutafuta nguvu za rohoni maana vita ya majini mapepo, na wachawi ni ya rohoni zaidi MUNGU AKUBARIKI SANA. NI MIM NDUGU YAKO KATKA KRISTO YESU MT S M MENDULO. KWA mawasiliano kwa ajili ya maombi na maombezi na. Mafundisho ya lnjili ya Yesu kuhusu ufalme wa mbinguni na msamaha kamili wa dhambi zote nipigie +255656995917 au email samendulo@gmail.com or Mlimamtakatifumistry@gmail.com. Tupo Kinondoni, Goba, Mabibo, NYOTE MNAKARIBISHWA Amen.