Zaburi 42:1

Kama paa atamanivyo maji ya kijito,ndivyo ninavyokutamani ee Mungu wangu...!!.

Zaburi 42:2

Naona kiu ya Mungu,kiu ya Mungu alie hai,nitafika lini kwake na kuuona uso wake..?.

Zaburi 42:3

Machozi yamekuwa chakula changu mchana na usiku,waliponiambiakila siku 'yuko wapi Mungu wako?'.

43:4

Nakumbuka tena mambo haya kwa majonzi moyoni mwangu:Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu,nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Mungu wakipiga vigelegele vya shukrani;umati wa watu wakifanya sherehe!.

Zaburi 42:5

Mbona nasononeka hivyo moyoni? Kwa nini nahangaika hivyo ndani mwangu? Nitamtumainia Mungu, maana nitamsifu tena yeye aliye msaada wangu na Mungu wangu

Friday, 26 February 2016

YESU ANAKUITA



Mwito wa Yesu ,(wito nikitendo cha kumsikia Mungu akitoa majukumu ya Utumishi wako)

Hadi unaitwa ujue ulikuwa kwenye mpango wa Mungu tangu hujazaliwa.

YEREMIA 1:5  Mungu ana sema , ?KABLA SIJA KUUMBA KATIKA TUMBO NALIKUJUA, NA KABLA HUJATOKA TUMBONI, NALIKUTAKASA; NIMEKUWEKA KUWA NABII WA MATAIFA. ?

Sasa basi hilineno lililomjja Yeremia lilikuwa ndiyo Yesu ( Neno=Yesu)

YOHANE 1:1-12 Point ipo 1:1?HAPO MWANZO PALIKUWEPO NENO,  NAYE NENO ALIKUWAKO KWA MUNGU, NAE NENO ALIKUWA MUNGU. ?

Hata leo Yesu anatuita tutende kazi yake yaani tutende mapenzi ya Baba.

YOHANA 6:38 Yesu anasema ?KWAKUWA MIMI SIKUSHUKA TOKA MBINGUNI ILI NIFANYE MAPENZI YANGU, BALI MAPENZI YAKE ALIE NIPELEKA.

Kama yeye amekuja kutimiza mapenzi ya Baba,  basi ni dhahiri kuwa anataka na wewe uyatimize vivyo hivyo,  yaani utumike kutimiza mapenzi ya Baba ila kupitia yeye.?

Mwitohuu hauchagui hali wala mali, bali yeyote atakaetii sauti hiyo, ZABURI 95:8 ?
MSIFANYE MIGUMU MIOYO YENU KAMA HUKO MERIBA KAMA SIKU YA MUSA JANGWANI,? mkisikia sauti ya Roho mtakatifu WAEBRANIA 3:7-8 ?KWAHIYO KAMA ANENAVYO ROHO MTAKATIFU, LEO KAMA MTAISIKIA SAUTI YAKE, MSIFANYE MIGUMU MIOYO YENU, KAMA WAKATI WA KUKASIRISHA , SIKU YA KUJARIBIWA KATIKA JANGWA,?

kumbuka Dhumuni kubwa ni wewe kutumika ili kazi ya Mungu ifanyike kupitia wewe YEREMIA 51:20-23, nitakuonesha mstar wa 20,?WEW U TLRUNGU LANGU NA SILAHA ZANGU ZA VITA,  KWA WEWE NITAVUNJA VUNJA MATAIFA ,  NA KWA WEWE NITAHARIBU FALME. ?

Katika wito huu pia Mungu anatuhakikishia usalama katika kutenda kazi nae ! YOSHUA 1:9 ?
JE!  SI MIMI NILIE KUAMURU?  UWE HODARI NA MOYO WA USHUJAA;USIOGOPE WALA USIFADHAIKE;KWAKUWA BWANA MUNGU WAKO,  YU PAMOJA NAWE KILA UENDAKO. ?

Nakila silaha ya kufanya kazi tunayo, 2PETRO 1:3 ?KWAKUWA UWEZA WAKE WA UUNGU UMETUKIRIMIA VITIVYOTE VIPASAVYO UZIMA NA UTAUWA, KWAKUMJUA YEYE ALIETUITA KWA UTUKUFUWAKE NA WEMA WAKE MWENYEWE?, Kwahiyo tunakila sababu ya kutii,  Yeremia alisema YEREMIA 1:6  ?NDIPO NILIPOSEMA, AA,  BWANA MUNGU! TAZAMA SIWEZIKUSEMA MAANA MIMI NI MTOTO?. na Mungu akamjibu YEREMIA 1:7-87-8 ?LAKINI BWANA AKANIAMBIA USISEME, MIMI NIMTOTO;MAANA UTAKWENDA KWA KILAMTU NITAKAE KUTUMA KWAKE, NAWE UTASEMA KILA NENO NITAKALO KUAMURU, USIOGOPE KWA SABABU YA HAO MAANA MIMI NIPO PAMOJA NAWE NIKUOKOE, ASEMA BWANA.?

Tujifunze kukubali wito na tusali sala ya kushukuru na kupokea ule wito tulio itiwa. Marium alipewa wito wa kuchukua mimba na kumzaa Yesu ambae leo nimkombozi wetu,  katika mwito ule yeye  ali uitikia na kuupokea kikamilifu,  LUKA 1:38 ?MARIUM AKASEMA ,  TAZAMA MIMI NI MJAKAZI WA BWANA NAIWEKWANGU KAMA ULIVYOSEMA . KISHA MALAIKA AKAONDOKA AKAENDA ZAKE.?  lakini tukirudi nyuma kidogo LUKA 1:26-37.  Utaona Marium aliuliza masali ili kufahamu wito wake kisawasawa,  hata wewe waweza kusali na kumuuliza Mungu ili akufunulie na kukufanya uujue,   Waefeso 1:17-23 point ipo kwenye 18, ?
MACHO YA MIOYO YENU YATIWE NURU, MJUE TUMAINI LA MWITO WAKE JINSI LILIVYO, NAUTAJIRI WA UTUKUFU WA URITHIWAKE KATIKA WATAKATIFU  JINSI ULIVYO?

Sasa basi Yesu anatuita kwenye wito ili tujenge kanisa ambalo yeye mwenye ndio kichwa cha kanisa lenyewe, WAKOLOSAI 1:18 ?
NAE NDIO KICHWA CHA MWILI YAANI CHA KANISA,NAYE NI MWANZO , NI MZALIWA WA KWANZA KATIKA WAFU, ILIKWAMBA AWE MTANGULIZI KATIKA YOTE. ?

Yesu alipotoka jangwani kujaribiwa alianza kwa kuwaita wale mitume Mathayo 4:18-21 ,  ambao waliongozana nae katika kutenda kazi, kazi yao kubwa ilikuwa kufanya kazi na Yesu pamoja na kujifunza kumjua Mungu kupitia Yesu,

Nahawa aliowateuwa kuwa mitume sio kama alibahatisha ila tayar walikwisha pangwa kutumika, ndio maana kwenye Yohana 17:12 ?,NILIPOKUWAPO PAMOJA NAO,  MIMI NALIWALINDA KWAJINALAKO ULILONIPA, NIKAWATUNZA;WALA HAPANA MMOJAWAPO ALIE POTEA, ILA YULE MWANA WA UPOTEVU ILI ANDIKO LITIMIE?.  tunaona akiwakabidhi kwa Mungu kama Baba alivyo mpa awajenge yeye akiwa kama mchungaji na mfano kwao nao wakatende kama yeye,

Kwahiyo mpendwa ili Yesu leo afanye kazi yake anakuhitaji wewe,

YESU AMEKUITA ILI UMTUMIKIE,
Somo na Mtumishi Shio Expery.

Thursday, 25 February 2016

ALHAMISI WIKI YA 2 YA KWARESMA





Somo: Yer 17:5-10  Zab: 2:1 1-2, 3-4, 6  Injili: Lk 16:19-31

Nukuu:

Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana,? Yer 17:5

Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake,? Yer 17:7

Mimi, Bwana, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake,? Yer 17:10

Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.? Lk 16:29,31

TAFAKARI:
Kuishi bila hofu ya Mungu; kutotimiza wajibu na kutokujali.?

Wapendwa wana wa Mungu, niwaalike tena kwa siku ya leo, tutafakari pamoja, ?kuishi bila hofu ya Mungu; kutotimiza wajibu na kutokujali.? Somo letu la kwanza laelezea hathari za kuishi bila kuwa na hofu ya Mungu. Injili yatuelezea hathari za kutotimiza wajibu na kutokujali.

Ndugu, tuanze safari yetu kwa kutafakari kwa undani hathari za kutokuwa na hofu yangu. Je, hofu ya Mungu ni nini? Mpendwa, hofu ya Mungu ni kuishi kwa kumtegemea Mungu kwa kila jambo. ?
Ee Bwana, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki,? Zab 40:5.

Ni kujenga mahusiano ya karibu na Mungu kiasi kwamba huwezi fanya lolote bila kumshirikisha Mungu. Ndugu yangu, ?mkabidhi Bwana kazi zako, na mawazo yako yatathibitika,? Mit 16:3. Mtu anayeishi katika hofu ya Mungu, upanga na Mungu, uwaza na Mungu, ushauriana na Mungu, na uyakabidhi maisha yake mwenyewe na mipango yake yote kwa Mungu. Huku ni kuishi katika baraka kama asemavyo Nabii Yeremia, ?Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake,? Yer 17:7

Kuishi bila hofu ya Mungu ni kujiamini kusiko fikirika. Ni kuamini na kutegemea vitu na mali, watu na vyeo vyao. Huku ndiko tunapochuma laana kama anavyosema Nabii Yeremia, ?Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana,? Yer 17:5. Mtu wa mwono huu kimaisha hawezi pata baraka. Mungu hana nafasi katika maisha yake. Na hapendi kumpa Mungu nafasi.

Mtu asiye na hofu ya Mungu huishi maisha linganishi mara zote. Mtu wa mtindo huu kimaisha hawezi jipokea alivyo; na hivyo ni vigumu kufanya mabadiliko kimwili na kiroho. Mtu wa mtindo huu awezi kuwa na furaha ya kweli. Muda wote huishi maisha ya ushindani na kusahau jambo lililo la msingi katika maisha yake, yaani, Mungu hupendezwa nawe kama ulivyo. Uwepo wake ulimwenguni hapa si bahati mbaya. Maisha bila Mungu ni sawa na samaki bila maji. Hivyo ni wajibu wangu na wako kuitafuta sura ya Mungu kila siku.?
Bali mimi nikutazame uso wako katika haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako,? Zab 17:15. Kwa nini basi itakupasa kuitafuta sura ya Mungu kila siku? Mtume Paulo anasema,?
Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni,? 1Kor 15:49. Na sura ya yule wa mbinguni ni UTAKATIFU. Ndugu yangu, bila Utakatifu hakuna mbingu. Kuitafuta Sura ya Mungu ni kuutafuta Utakatifu na kuuishi huo utakatifu tungali hai kila mmoja wetu kadiri ya mazingira na wito wake.

Furaha ya kweli haipatikani kwa mali tulizonazo; bali twaipata kwa kujipokea kama tulivyo na kujua upendo wa Mungu ndani yetu. Yeye Mungu yupo tayari kutupokea na kutufanya tena wana wake tunapokiri kupotoka kwetu na kumuasi. Mungu huturudishia hadhi yetu na mastahili yetu kama watoto wake. Hii ndiyo furaha ya kweli ndani mwetu. Hakuna mamlaka yoyote au binadamu yeyote awezaye kuyafanya haya. Ni Mungu tu.

Somo la Injili la tupa kisa cha tajiri na maskini Lazaro. Tajiri anajulikana kwa mwono wake, na maisha yake ya anasa. Lazaro anajulikana kwa jina lake, umaskini wake na unyonge wake. Kosa kubwa la tajiri huyu ni dhambi ya kutotimiza wajibu. Ndugu yangu, kabla ya kuendelea na tafakari hii nikuombe usali kwanza sala ya ?NAKUUNGAMIA.? Dhambi ya kutotimiza wajibu, ni kosa la nne tunalokiri katika sala hii ya ?nakuungamia Mungu mwenyezi.? Lazaro tunaambiwa mara zote alikaa kwenye mlango, ikimaanisha kwamba kwa vyovyote vile tajiri huyu alimwona Lazaro katika dhiki yake na ilimpasa tajiri huyu afanye kitu. Kutotimiza wajibu, ni kosa la kutokufanya kitu wakati ulitakiwa kufanya kitu. Tajiri huyu anahukumiwa kwa kutokujali na kutokufanya chochote.

Ndugu yangu, tazama mazingira unayoishi, Je, akina Lazaro hawapo? Wale Mungu aliotubariki kuwa na Magari binafsi, Je, unapofunguliwa geti hujamwona Lazaro pembeni akisubiri wema na upendo wako? Wale ambao hula vizuri kila siku na asubuhi kumwaga viporo vya wali na vipande ya samaki, Je, huwaoni akina Lazaro wakilichungulia shimo taka kwa masikitika? Wewe ambaye kila siku huingia ofisini na mkoba wako, Je, humuoni Lazaro kwenye benchi akisubiri wema na huruma yako?

Ukweli ni kwamba, wote tutakufa na kujongea kiti cha ukumu. Tunapoishi hapa duniani, tunaaswa na mzaburi, ?usiogope mtu atakapopata utajiri, na fahari ya nyumba yake itakapozidi. Maana atakapokufa hatachukua cho chote; utukufu wake hautashuka ukimfuata,? Zab 49:16-17. Mambo yote yatupayo ufahari ipo siku tutayaacha. Je mbele ya Mungu tutafika na jambo gani kama utambulisho wetu?

Ndugu yangu, ijumaa ijayo, nakualika wakati wa njia ya msalaba utafakari kituo cha tisa; Yesu anaanguka mara ya tatu. Njia ya msalaba kwa kutumia misale ya waamini, kuna maneno haya katika kituo hiki cha tisa; ?Mara nyingi mno ninajibovusha kwa kupenda mno starehe, anasa na tafrija. Ee Yesu mwema, nisaidie kuufuata mfano wa Mtakatifu Paulo, niutese mwili wangu na kuutumikisha, ili nipate siku moja tuzo mbinguni.? Katika kujibovusha huko, hujakutana na akina Lazaro?

Tunapojitesa na kuwajali wengine, hakika tutapata tuzo mbinguni. Mateso aliyoyapata Tajiri, alitamani na kuomba taarifa zile ziwafikie ndugu zake ili wasije patwa na mateso yale. Ibrahimu anamjibu, ?Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu.? Lk 16:29,31. Ndugu yangu, hapa Musa anawakilisha Sheri za Mungu na Amri zake. Manabii hapa ni wale wahudumu wa neno la Mungu. Kwa maana nyingine tungesema, sisi kama wafuasi wa Kristo tunajua taratibu zitupasazo kuishi, ikiwa ni pamoja na Amri za Mungu. Na Amri kuu kupita zote ni Amri ya upendo.?
Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii,? Mt 22:37-40 Pili, tumepewa wachungani, na wapo muda wote kwa kutuhudumia hasa kiroho. Tunaonywa na kufundishwa kupitia mahubiri yao. Kwa kuyashika haya mawili na kuyaishi, basi tuzo tutalipata. Nje ya hapo tutegemee mateso makali.

WEWE NI HEKALU LA ROHO MTAKATIFU

Mpendwa katka Bwana ninakusalimu kwa jina la Bwana Mungu wa majeshi
     Wakorintho 6:19-20
Au hamjui kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Mlinunuliwa kwa thamani kubwa bas sasa mtukuzeni Mungu katka miiili yenu.
Kitendo cha kumkana shetani nakumchagua Yesu kua Bwana na mokozi wa maisha yako Unafanyika kua hekalu la Roho Mtakatifu, kwakua huyo Roho anaanza kuishi ndani yako, mtu ambaye amempokea Yesu haimpaswi kutenda dhambi kwakua unapompokea Yesu mwili wako unakufa na roho yako lnafufuka, kwamaana mtu asimjuwa Mungu anaongozwa na mwili, lakin mtu anayemjua Mungu huongozwa na Roho. Ndani ya Mtu kunna vitu vitatu Mwili, Roho, Na Nafsi. Shetani anasmama katka mwili, wakat Mungu anakaa katka Roho vitu hivi viwili Mungu na shetani wanapigana vita kwa ajili ya Nafsi, kwakua ndani ya Nafsi ndiko kuna uhai, ufahamu, utashi, na aKili, lakin pia Maamuzi ya jambo lolote.
MAPIGANO YA MWILI NA ROHO.
kwakua sababu mwili hutaman ukishindana na roho na roho hushindana na mwili, kwa maana hiz zinapigana hata hamwez kufanya mnayotaka. Wagalatia 5:17
Mtu ana mwili , nafsi na roho, mwili ni udongo uliyopuliwa pumzi nakuwa hai, baada ya mtu kufa hurudia hali yake ya udongo. Lakin  Roho hii lmetoka kwa Mungu, nayo lnatabia ya uMungu. Na hii roho ndio mwanadamu atakayeishi milele, lwe ni mbinguni au Jehanamu hiyo ltategemea matendo yako ulipokua dunian ulikua unafanya nin
Kwamaana Roho lnatabia yakuishi maisha ya kumpendeza Mungu kwakua lnajua lsipoishi maisha yakumpendeza Mungu mwisho wake ni Jehanamu.
Lakin tunda la roho ni upendo, furaha, amanu, uvumilivu, utu wema, fadhiri, uaminifu, upole kiasi, juu ya mambo kama hayo hakuna sheria Wagalatia 5:22-23
Mwili unafahamu yakua mwisho wake ni hapa hapa dunian, hivyo mwili hutamani ya dunia zaid na shetani naye huuteka mwili ili kulazimisha nafsi kutenda dhambi. Mwili hauna juhudi yoyote yakuifanikisha roho kwenda mbinguni, na ndio maana kuna ushindani mkubwa kati ya mwili wenye tabia zadunia, na roho yenye tabia za mbingu.
Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndyo haya Uasherati,, uchafu, ufisadi, lbada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu hasra, fitina faraka, uzushi, husuda...... endelea Wagalatia 5:19-20.
Hivyo mwili unataka matendo ya mwili ndio yatendeke wakat roho lnataka matendo roho ndio yatendeke. Biblia lnasema atendaye dhambi ni wa lbilisi, kwa maana matendo ya KiMungu ni mema kama lilivyo tunda la roho.

KAA UKIJUA HILI
Vita vya kiroho havipo mbali vipo ndani yako kat ya mwili na roho, kwa maana yakwamba roho lkiushinda mwili katka matendo Mungu anachukua nafasi ndani yako, hivyo lile tunda la roho linageuka Roho Mtakatiifu ambaye anamuru naffsi kutenda yaliyo mema kila ukitaka kkutenda mabaya Roho mtakatifu anakujulisha kuhusu jmbo hilo baya hivyo ndani yako unakua na Hofu ya Mungu huwezi kutenda dhambi.
Lakin mwili ukishinda roho shetan anaingia ndani yako hivyo analeta mawakala wake ndani yako, kama mapepo wa baya au majini, hivyo viumbe hawa wanaingoza nafsi kutenda maovu. Kwamaana nafsi lnakua lmetekwa na matokeyo yake ni dhambi. Kwa maana mtu anakua katka hali yakutojielewa kwamaana anaongozwa na roho waovu hawa. Anachofanya shetani anapanda jambo ndani ya mtu, anaweza kuweka roho ya ujambazi, ushoga, Uzinzi, unafiki na mengineyo Mungu awabariki sana.
Samuel M Mendulo.
Samendulo@gmail.com.
 facebook Samuel Mendulo.
 Namba +255656995917

Tuesday, 23 February 2016

UZIMA WA MILELE.


    Yohana 17:1-10

Maana ya uzima= Nihali ya kuwa na afya njema.
Maana ya Milele= Ni bila kua na mwisho.
Lazima kujua kua mtu anaanza kuishi maisha ya uzima akiwa dunian, ili kutengeneza maisha ya uzima wa milele nilazima huyu mtu awe nao uzima wa kimwili ambao ni maisha ya dunian. Lakin ukweli nikwamba maisha ya uzima wa milele yanaanzia dunian. Neno uzima wa milele linamaana pia ya Maisha baada ya kifo. Wokovu upo duniani kwa njia ya Yesu kristo baada ya kufa ni hukumu. Nimekua nikisikia wachungaji wakiomba kwa namna yaajabu ambayo sikupata kuelewa. Wengine wakisema sadaka ambayo wametowa watu wakat wa lbada ya mazishi lmtakase marehemu ili apate kusamehewa dhambi, lakin huu ni uongo ambao hauna mantiki yoyote kwa maana mtu anapokufa kinachofuata nikusubiri hukumu, Usije ukaamini hata siku moja kwamba maombi yako yanaweza kubadilisha hali ya marehemu akawa msafi hapo utakua unajidanganya. Au ukawa na wazo kwamba usipookoka na kuishi maisha matakatifu basi ukifa mchungaji, au mtumishi wa Mungu akikuombea wewe utatakasika nakupata uzima wa milele hiyo nayo ni ndoto ya mchana. Wakat wakutengeneza maisha ya baadae kwa maana ya maisha baada ya kifo ni sasa au msisha ya uzima wa milele, Kwa maana biblia lnasema Wokovu ni sasa hivyo lazma kuokoka na kudumu katka maisha ya kumpendeza Mungu kama unania ya kupata uzima wa milele.
  Yohana 10:14-17
Mstr wa (10) Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu, Mim nalikuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele
Neno hili mpendwa linatupa uhakika yakwamba Yesu alikuja ili tuwe na uzima kwa maana ya afya njema. Mwivi ni shetani ambaye analeta magonjwa kinyume na mpango wa Yesu wakutupa uzima tena sio uzimatu bali uzima tele. Kwasababu biblia lnasema lli litimie lile neno lililonenwa na nabii lsaya akisema
Mwenyewe aliutwa udhaifu wetu,  Na kuyachukua Magonjwa yetu Mathayo 8:17 Maana yake nikwamba ukiwa ndani ya Kristo Yesu ni marufuku kuumwaumwa kwamaana aliyachukua magonjwa yetu nayo yakawa ya kwake na kwa kupigwa kwake tumepona. Hii ndio maana ya uzima kwa maana ya afya njema. Tatizo tulilokua nalo pale magonjwa yanapokuja tunakimbilia kufadhaika na kulalamika lakin magonjwa ni mpango wa shetan kwa ajili ya kuwatesa wana wa Mungu lakin jambo hili Mungu alilijua mapema na ndio maana maandiko yako wazi. Kama unaumwa umapaswa kutumia vifungu kama hivi kudai hali yako ya uzima na Mungu lazma atakuponya kwamaana yeye hapinngani na neno lake, unapodai lazima alitimize lakin kudai huku nilazma pia uwe nayo haki kwa maana ya matendo mema maana Mungu hasikilizi maombi ya mwenye dhambi, hivyo kabla yakudai haki lazma ufanye toba kwamaana ya kujitakasa.

  UZIMA WA MILELE
Kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliyompa awape uzima wa milele
Mstr huu unatuonyesha yakwamba Mungu alimpa Yesu mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili awape uzma wa milele, maana yake uzima wa milele unaishi ndani ya Kristo Yesu. Na ndio maana unapompokea Yesu ndio chanzo cha uzima wa milele, pale ndipo unaanza kutengeneza maisha ya baada ya kifo, yan uzma wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujuwe wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. Yohana 17:1-3 Yesu ndio anatupa uzima wa milele lakin kumjua Mungu wa kweli na Yesu ambaye alitumwa kwetu ili kutupa huo uzima wa milele. Kwa njia ya msalaba. Ninakueleza kwa jina la Bwana yakwamba kumjua Mungu ndio uzma wa milele kwa maana ukimjua Mungu utaishi maisha yanayoendana na Mungu. Yohana

Biblia lnasema Twajua yakua mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi bali yeye alizaliwa na Mungu hujilinda ukisoma 1 Yohana 5:18-21 biblia lko wazi kwamba kama umeokoka huwez kutenda dhambi kwa maana unajua jinsi ya kujilinda kwasababu Huyu Yesu anakaa ndani yako. Hivyo kama unahiraji uzma wa milele lazma ujilinde na uovu. Na kama unafanya basi uache kabisa laazma ujuwe hakuna dhambi ndogo wala kubwa zote ni dhambi. Ubarikiwe sana
Somo limeandaliwa na Mtumishi Samuel M Mendulo
                                              Samendulo@gmail.com
                                              Namba +255656995917 Amen

Monday, 22 February 2016

Juma la 2 la Kwaresma, Jumapili 21 Februari 2016


Somo la 1
Mwa. 15:5-12, 17-18

Mungu akamleta Ibrahimu nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.

Kisha akamwambia, Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi. Akasema, Ee Bwana Mungu, nipateje kujua ya kwamba nitairithi? Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa. Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua. Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza.

Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama. Siku ile Bwana akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati.

Neno la Bwana? Neno la Bwana.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 27:1,7-9, 13-14 (K) 1

(K) Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu.

Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope nani?
Bwana ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu nani? (K)

Ee Bwana, usikie kwa sauti yangu ninalia,
Unifadhili, unijibu.
Moyo wangu umekuambia,
Bwana uso wako nitautafuta. (K)

Usinifiche uso wako,
Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira.
Umekuwa msaada wangu, usinitupe,
Wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu. (K)

Naamini ya kuwa nitauona wema wa Bwana
Katika nchi ya walio hai.
Umngoje Bwana, uwe hodari,
Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana. (K)

SOMO 2
Flp. 3:17-4:1

Ndugu zangu, mnifuate mimi, mkawatazame wao waendao kwa kuufuata mfano tuliowapa ninyi. Maana wengi huenenda, ambao nimewaambieni mara nyingi habari zao, na sasa nawaambia hata kwa machozi, kuwa ni adui za msalaba wa Kristo; mwisho wao ni uharibifu, mungu wao nit umbo. Utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani.

Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Basi ndugu zangu, wapendwa wangu, ninaowaonea shauku, furaha yangu, na taji yangu, hivyo simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu.

Neno la Bwana? Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO
Mt. 17:5

Sauti ya Baba ilitoka katika wingu jeupe: ?Huyu ni Mwanangu mpendwa wangu, msikieni yeye.?

INJILI
Lk. 9:28b-36

Yesu aliwatwaa Petro na Yohane na Yakobo akapanda mlimani ili kuomba. Ikawa katika kuomba kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta. Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya; walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemu. Petro na wale waliokuwa pamoja na walikuwa wameelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka walikuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye.

Ikawa hao walipokuwa wakijitenga naye, Petro akimwambia Yesu, Bwana mkubwa, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya; hali hajui asemalo. Alipokuwa akisema hayo lilitokea wingu likawatia uvuli, wakaogopa walipoingia katika wingu hilo.

Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye. Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yup eke yake.

Nao wakanyamaza, wasitangaze kwa mtu siku zile lolote katika hayo waliyoyaona.

Wednesday, 17 February 2016

Juma la 1 la Kwaresma, Jumanne 16 Februari 2016



Somo la 1
Isa. 55:10-11

Bwana asema: Kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko: bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

Neno la Bwana? Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 34:3-6, 15-18 (K)17

(K) Wenye haki, Bwana anawaponya na taabu zao zote.

Mtukuzeni Bwana pamoja nami,
Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
Nalimtafuta Bwana akanijibu,
Akaniponya na hofu zangu zote. (K)

Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,
Wala nyuso zao hazitaona haya.
Maskini huyu aliita, Bwana akasikia,
Akamwokoa na taabu zake zote. (K)

Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
Na masikio yaje hukielekea kilio chao.
Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya,
Aliondoa kumbukumbu lao duniani. (K)

Walilia, naye Bwana akasikia,
Akawaponya na taabu zao zote.
Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo,
Na waliopondeka roho huwaokoa. (K)

SHANGILIO
Zab. 95:8

Leo msifanye migumu mioyo yenu, lakini msikie sauti yake Bwana.

INJILI
Mt. 6:7-15

Siku ile Yesu aliwaambia wafuasi wake: Mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. Basi ninyi salini hivi:

Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.

Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Neno la Bwana?

Monday, 15 February 2016

Juma la kwanza la Kwaresma


Jumatatu 15 Februari 2016
Somo la 1
Law. 19:1-2, 11-18

Bwana akanena na Musa, akamwambia, Nena na mkutano wote wa wana wa Israeli, uwaambie, Mtakuwa watakatifu; kwa kuwa mimi Bwana, Mungu wenu, ni mtakatifu.

Msiibe, wala msidanganye, wala msiambiane uongo. Msiape uongo kwa jina langu, hata ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi Bwana. Usimdhulumu jirani yako, wala kumnyang?anya mali yake; ijara yake aliyeajiriwa isikae kwako usiku kucha hata asubuhi. Usimlaani kiziwi, wala usitie kwazo mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako; Mimi ndimi Bwana. Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki. Usiende huko na huko katikati ya watu wako, kama mchongezi; wala usisimame kinyume cha damu ya jirani yako; Mimi ndimi Bwana. Usimchukie ndigu yako moyoni mwako; ni lazima kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake. Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako nafsi yako; Mimi ndimi Bwana.

Neno la Bwana? Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 19:7-9, 14 (K) Yn. 6:64

(K) Bwana unayo maneno ya uzima wa milele.

Sheria ya Bwana ni kamilifu,
Huiburudisha nafsi.
Ushuhuda wa Bwana ni amini,
Humtia mjinga hekima. (K)

Maagizo ya Bwana ni ya adili,
Huufurahisha moyo.
Amri ya Bwana ni safi,
Huyatia macho nuru. (K)

Kicho cha Bwana ni kitakatifu,
Kinadumu milele,
Hukumu za Bwana ni kweli,
Zina haki kabisa. (K)

Maneno ya kinywa changu,
Na mawazo ya moyo wangu,
Yapate kibali mbele zake, Ee Bwana,
Mwamba wangu, na mwokozi wangu. (K)

SHANGILIO
Zab. 51:1-10, 12

Ee Mungu, uniumbie mioyo yenu; Unirudishie furaha ya wokovu wako.

INJILI
Mt. 25:31-46

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kodnoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.

Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme, mliowekewa tayari tangu kuubwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha? Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika? Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake; kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe; nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa na kifungoni, msije kunitazama.

Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie? Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi. Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Neno la Bwana...!!

MTAFUTE KWA BIDII ABADILI MAISHA YAKO

Shalom!! Neema na lwe kwako, na rehema na aman, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana na mwokozi wetu Amen.
 
  LUKA 19:1-10
BWANA YESU APEWE SIFA!!!
 Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake, na tazama palikua na mtu jina lake Zakayo mkubwa mmoja katika watoza Ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikua akitafuta kumuona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwasababu ya umati wa watu maana ni mfupi wa kimo.....!
 Mpendwa katka Kristo Yesu, biblia inaeleza kuhusu habari za mtu mmoja jina lake Zakayo naye alikua mtoza ushuru hii ni kazi ambayo alikua anafanya. Lakin pia alikua tajiri, maana yake alikua na kila kitu haswa kuhusu mahitaji ya kimwili, alikuwa amejitosheleza. Lakin mtoza ushuru huyu na tajiri alitaka kumuona Yesu ni mtu wa namna gani, huyu hakua na maombi wala mahitaji kwa Yesu bali alitaka kumuona ni mtu wa namna gani kwamaana alipata habari zake,
 Bwana Yesu apewe sifa..!! Mstr wa 4 Akatangulia mbio akapanda juu ya mkuyu apate kumwona kwa kua atakuja kupitia njia ile. Zakayo alitaka kumwona Yesu lakin kukawa na kikwazo umati wa watu ulikua mkubwa sana naye alikua mfupi wa kimo, alijua kama sijatafuta njia nyingine mim Yesu sitamwona, akaumiza kichwa kufikiri afanyeje lakin mwisho akapata jibu akaona apande kwenye mkuyu. Biblia lnasema akatangulia mbio akapanda juu ya mkuyu, maana yake alikimbia ili kuwai kabla watu hawajafika eneo la mti lakin pia kwakua nimfupi lazima kulikua na kikwazo pia kwenye kupanda juu ya mti huenda aliomba msaada ili apandishwe, Mpendwa mim sijui nikikwazo kinakukwamisha ili kumuona Yesu Kristo lakin hapa tunaona jinsi ambavyo Zakayo alikabiliana na kikwazo chake, kama huwez kupanda kwenye mtii je! Umeomba watu wakupandishe? Kwa maana Zakayo alipopata jibu la kukabiliana na kikwazo cha ufupi wa kimo alikutana na kikwazo cha jinsi yakupanda kwenye mti bila shaka unajua watu wafupi wanavyopata shida kupanda mahali ambapo ni palefu. Je! Wewe na mim tumekwama wapi? Mstr wa 5 Na Yesu alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambiah Zakayo shuka upesi kwakua leo lmenipaswa kushinda nyumbani mwako HALELUYAAAA!  Zakayo aliangaika kumtafuta Yesu ili amuone akatumia mbinu mbadala kumbe wakat anahangaika Yesu naye alikua anamtafuta. Ninakwambia kwa jina la Yesu kristo Kristo kuhangaika kwako sio bure kwamaana huyo Yesu naye yupo njian haijalishe unapita kwenye mazingira gan kwa maana hata Zakayo alipitia vikwazo lakin aling'ang'ana na mwisho alifanikisha ndoto yake na sio kufanikisha kumuona tu alipata nafasi ya Yesu kuingia nyumbani mwake. Biblia lnasema akafanya haraka akashuka akamkaribisha kwa furaha! Mstr wa 7 unasema hata watu walipoona walinung'unika wote wakisema ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi, huenda na wewe unakutana na mambo kama haya watu wanadai wewe ni mwenye dhambi lakin angalia baada ya Yesu kuingia nyumban mwa Zakayo maisha ya Zakayo yalibadilika ghafla Zakayo alijitambua kwamba matendo mengi ni kinyume na Yesu naye akasema mstr wa 8 Zakayo akasmama akamwambia Bwana,  Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskin na lkiwa nimemnyang'anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne, Toba safi kabisa maisha ya Zakayo yalibadilika baada ya kumtafuta Yesu kwabidii na kumuona. Mstr wa nane Zakayo anaomba toba tena anaambatanisha na sadaka ambayo ni nusu ya mali yake, lakkn haishii hpo anarudisha vitu alivyokua ananyang'anya kwa hila wakat anatoza ushuru, lakin hayo yote nibaada ya Zakayo kukabiliana na vikwazo vingi, Wewe na mim ndio Zakayo wa leo tunapitia magumu mengi katika kumtafuta huyu Yesu vikwazo ni vingi saa nyingine afadhari ya Zakayo maana yeye allikua tajiri lakin lipo tumaini kubwa juu yetu mpendwa kwamaana kuhangaika kwetu sio bure naye Yesu yu karibu atakutowa katka hiyo hali nawe utang'aa kama nyota gizan kwa maana Yesu alipoingia nyumbani mwa Zakayo alibadili maisha yake! Na mstr wa 9 Yesu anasema leo Wokovu umefika nyumbani humu kwa sababu huyu nae ni mwana wa lbrahimu. Mstr wa 10 anamaliza kwakusema kwakua Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea. Ni maombi yangu kwako Uendeleye kumtafuta huyu Yesu kwamaana ninao uhakika yakwamba atajibu kile kilio chako hata kama utaona anachelewa lakin wewe endeleya kumuita na kumtafuta tena kwa bidii kikwazo kisikufanye wewe kuishia njian bali pigana mpaka kieleweke.
 Ubarikiwe sana
 Ameeen!!!!

Wednesday, 10 February 2016

Mabadiliko ya ratiba ya Maombi kituo cha Mabibo

Wapendwa katika Kristo,tunapenda kuwafahamisha kuwa kutokana na kuanza kwa kipindi cha Kwaresma,ratiba ya maombi mabibo imebadilika badala ya ijumaa saa kumi na nusu,maombi yatakuwa yanafanyika kila jumatatu mda ule ule ili kuwaruhusu wenzetu wakatoliki waweze kuhudhuria ibada ya njia ya msalaba kila siku ijumaa.
 <<<...TUNAWATAKIA MFUNGO MWEMA WA           KWARESMA....>>>

Monday, 8 February 2016

Leo natamani mpate somo zuri

Mwana WA mungu Kuna hatua Tatu za ukuaji 1 kuwa mtoto kiroho 2 mwana wa mungu 3 kuwa mlithi na mwana wa mungu 1 kuwa mtoto kiroho yohana 1:12-13 Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika kuwa watoto wa mungu, Kwahiyo hii ni atua ya kwanza ya wokovu unapompokea yesu una kuwa mtoto inabidi ukae chini ufundishwe katika mambo ya mungu akuna habari za kuibuka hapana lazima ufundishwe ndio usimame ukiwa kama mtoto mungu uwa anakupa msahada mwingi maana kama kuku anavyo angalia watoto wake ndivyo mungu anavyo kuangalia wewe Pia sipendi mkose katika huu mstali WA kumi na Tatu Mahana awakuzaliwa kwa mapenz ya MTU wala ya mwili Bali mungu Kuna watu wengine wanaomba kwa akili zao wenyewe mtu anayaona yanamzunguka ndio anaomba Hayo ni mapenzi ya mwili wengine wamezaliwa kwa mapenzi mtu Wengi wameenda kwa waganga WA kienyeji ili kupata watoto harafu wanasema wamepewa na mungu ilo hakuna hayo ni mapenz ya mganga WA kienyeji uwezi kusema unaenda kwa mganga harafu unasema aliyejibu mungu huo ni uongo na mtoto hatakaye zaliwa hatakuwa nusu mtu nusu shetani Ngoja tuangalie kuwa mwana wa mungu Warumi 8:14 Wanaoongozwa na roho wa mungu hao ndio wana wa mungu 1,roho wa awezi kukuongoza kwenye uzinzi wengi wa wamefanya dhambi wamesema wameongozwa mungu awezi kukuongoza kwenye dhambi 2,wengi wamesimamia maandiko kusema kusema mungu ametuongoza kumbe uongo,kunywa pombe na kusema yesu alitengeneza pombe,kutumia maandiko kwenye uzinzi na kusema hata ibrahimu alifanya kwa mjakazi wake na ruksa hakiona mkewe hazai unapoongozwa na mungu unaenda mema tena roho wa uwangoongoza watu wake kwenye kufanya huduma yohana 14:12-14 Ukijaa roho mtakatifu utafanya vitu kwa mapenzi yako mwenyewe Tutaendelea,,,